Katibu na Mshauri Mkuu wa Sheria wa Makampuni
ya IPTL na PAP, Bw. Joseph Makandege (kushoto) akimkabidhi balozi wa
kujitolea wa Imetosha Foundation, Henry Mdimu mfano wa hundi ya shilingi
milioni 10 fedha waliyoitoa kusaidia harakati za imetosha jana jijini Dar
es Salaam Balozi wa kujitolea wa
Imetosha Foundation, Henry Mdimu (kulia) akizungumza na wanahabari kwenye
hafla fupi ya kukabidhiwa shilingi milioni 10 zilizotolewa na Makampuni ya
IPTL na PAP kusaidia kampeni maalumu kupinga mauaji ya watu wenye albino.
Kushoto ni Katibu na Mshauri Mkuu wa Sheria wa Makampuni ya IPTL na PAP,
Bw. Joseph Makandege. Katibu na Mshauri Mkuu wa Sheria wa Makampuni ya IPTL na
PAP, Bw. Joseph Makandege (wa pili kulia) akizungumza na wanahabari katika
hafla ya kukabidhi hundi ya shilingi milioni 10 kusaidia harakati za
imetosha jana jijini Dar es Salaam. Wa kwanza kushoto ni Balozi wa
kujitolea wa Imetosha Foundation, Henry Mdimu. Baadhi ya viongozi na wajumbe wa kamati
ya utendaji ya Imetosha Foundation wakipiga picha na hundi ya shilingi
milioni 10 fedha iliyotolewa na Makampuni ya IPTL na PAP kusaidia kampeni
maalumu kupinga mauaji ya watu wenye albino. Wa kwanza kushoto ni Katibu na
Mshauri Mkuu wa Sheria wa Makampuni ya IPTL na PAP, Bw. Joseph Makandege. Balozi wa kujitolea wa
Imetosha Foundation, Henry Mdimu (kulia) akizungumza na wanahabari kwenye
hafla fupi ya kukabidhiwa shilingi milioni 10 zilizotolewa na Makampuni ya
IPTL na PAP kusaidia kampeni maalumu kupinga mauaji ya watu wenye albino.
Kushoto ni Katibu na Mshauri Mkuu wa Sheria wa Makampuni ya IPTL na PAP,
Bw. Joseph Makandege.
Na Mwandishi Wetu
KAMPENI maalumu za kupinga mauaji ya watu wenye u-albino
nchini inayojulikana kama 'Imetosha' iliyoanzishwa na balozi wa kujitolea,
Henry Mdimu, chini ya Imetosha Foundation zimezidi kushika asi baada ya
makampuni ya IPTL na PAP kutoa shs milioni 10 kusaidia kampeni hizo.
Katibu na Mshauri Mkuu wa Sheria wa Makampuni ya IPTL na PAP, Bw. Joseph
Makandege jana alimkabidhi balozi Mdimu mfano wa hundi yenye thamani ya
shilingi milioni 10 kama ishara ya kuunga mkono kampeni hizo za kutoa elimu
kutokomeza imani potofu zilizojengeka kwa baadhi ya wanajamii juu ya watu
wenye albino.
Akizungumza katika hafla hiyo fupi Bw. Makandege alisema matukio ya mauaji
au kukatwa viungo kwa watu wenye ulemavu wa ngozi yaani albino yamefika
hatua ya kutisha nchini Tanzania, hususani katika kanda ya ziwa hivyo kuna
kila sababu kila mmoja bila ubaguzi kushiriki kusaidia mapambano hayo.
Alisema ulemavu wa ngozi waliyonao watu wenye albino ni mapungufu ya
kibaiolojia ambayo ni mapenzi ya Mungu hivyo imani potofu zinazoendelea
hazina budi kupigwa vita kwa nguvu zote.
"...Kuna minongono mitaaani kwamba watu wanatenda matukio hayo wana imani
potofu kwamba ukitumia kiungo cha mtu mwenye albinism, ndipo utafanikiwa.
Kama kweli viungo vyao vingekuwa vinaleta utajiri, basi watu wenye albinism
wangekuwa matajiri namba moja duniani," alisema Makandege akizungumza.
"...Sisi IPTL na PAP tumeguswa sana na jambo hili. Kwa wote wanaofanya
matendo haya, mnapaswa kuwa na hofu ya Mungu mkijua kuwa siku ya kihama,
kila mtu atajibu na kuhukumiwa kwa matendo yake. Tunakubaliana kabisa na
wenzetu IMETOSHA Foundation kwamba, imefika wakati kila Mtanzania, na hata
wageni waishio Tanzania, kusema IMETOSHA na kusimama kidete kuwalinda hawa
ndugu zetu," alisisitiza kiongozi huyo wa IPTL.
Aidha kampuni za IPTL na PAP zimeyataka makampuni mengine nchini na watu
binafsi kuungana kwa kuchangia harakati hizi za imetosha ili kusaidia
kampeni ya imetosha kupita mikoa ya kanda ya ziwa kupaza sauti na
kuielimisha jamii juu ya uwepo wa imani potofu zinazoendeleza mauaji ya
watu wenye u-albino.
Kwa upande wake Balozi wa Imetosha, Mdimu aliishukuru kampuni za IPTL na
PAP kwa moyo wauliouonesha wa kusaidia harakati hizo na kumtaka kila
Mtanzania kwa nafasi yake kusaidia kupaza sauti kwamba imetosha mauaji na
unyanyasaji wanaoupata watu wenye ualbino. Alisema mauaji haya yanamgusa
kila Mtanzania na kuendelea kuichafua nchi yetu hivyo kumtaka kila mmoja
kupaza sauti yake kupinga vitendo hivyo.
Machi 28, 2015 Imetosha Foundation inatarajia kufanya matembezi ya hisani
kuchangisha fedha zaidi ili kusaidia kampeni za kukomesha mauaji ya watu
wenye u-albino kabla ya kuanza rasmi safari za kuzunguka katika mikoa ya
kanda ya ziwa pamoja na wasanii waliojitolea kueneza elimu hiyo kwa jamii
moja kwa moja.
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia