UHURU FM 95.7 FM WAFANYA BONGE LA PATI KUUKARIBISHA MWAKA MPYA

Wafanyakazi wa Uhuru FM, Redio ya wananchi wakiongozwa na Dj Fast Edie (kushoto) wakishow love wakati wa tafrija yao ya kuukaribisha mwaka mpya iliyofanyika Februari 27, 2015 katika ukumbi wa Tukuyu katika Hoteli ya Land Mark jijini Dar es Salaam. 

Tafrija hiyo iliyoongozwa na Kaimu Mkurugenzi wao Angela Akilimali ilifana na kupongezwa na kila mfanyakazi kwa jambo hilo jema la kuwakutanisha wafanykazi na kufurahi pamoja. 
Kaimu Mkurugenzi wa Uhuru FM, Angela Akilimali akizungumza machache wakati wa tafrija hiyo. Pamoja na mambo mengine aliwaasa wana Uhuru FM, Redio ya Wananchi kuzingatia weledi katika utekelezaji wa majukumu yao hasa katika kipindi hiki cha Kura ya maoni ya katiba mpya pamoja na Uchaguzi mkuu.
 Picha ya pamoja ya wafanyakazi na wageni waalikwa katika tafrija hiyo.
 Viongozi wa Juu wa Uhuru FM, wakiongozwa na Kaimu Mkurugenzi, Angel Akilimali (katikati).
 Burudaaaaaaniii ilitawala.
 Ni balaaa hakuna aliyekubali kukaa chini... na mambo ya Msondo hayo.
Ilikuwa ni fulu rahaaa kwa wana Uhuru FM

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

Previous Post Next Post