Bendi ya muziki wa dansi ya jijini dar es salaam skylight Band kwa mara ya kwanza inatarajia kutua jijini Arusha kufanya show ya nguvu usiku wa pasaka
Akiongea na waandishi wa habari muandaaji wa onyesho hilo Erinest alisema kuwa bindi hiyo inakuja kwa mara ya kwanza jijini hapa kwa ajili ya kuwapa burudani wakazi wa jiji hili na vitongoji vyake.
Aliwataka mashabiki wa muziki wa dansi nchini kujiandaa kushuhudia onyesho hilo linalotarajiwa kuwa la kihistoria .
" napenda kuwaambia wapenzi wa muziki wa dansi wajiandae kupata burudani ya aina yake katika usiku huu wa siku kuuu ya pasaka"alisema Erinest