Na Malisa GJ,
Mwishoni
mwa juma lililopita uliibuka mjadala juu ya kauli za baadhi ya viongozi
wa juu wa CHADEMA kuhusiana na kufutwa uanachama kwa Mbunge wa
Kaskazini Mhe.Zitto Kabwe.
Mjadala mkubwa ulikua juu ya kauli za wabunge watatu wa CHADEMA ambao ni Mhe.Tundu Lissu, Halima Mdee na Ezekia Wenje.
Mjadala
ulianza baada ya Lissu kueleza msimamo wa Katiba juu ya hatma ya
mwanachama aliyefungua kesi mahakamani dhidi ya chama na akashindwa. Je
nini kinatokea?
KWANINI LISSU ALIKUA SAHIHI.
Lissu
alieleza msimamo wa Katiba. Alichokisema Lissu si mawazo yake. Ingekuwa
mawazo yake bila shaka hata mimi ningempinga, lakini kwa kuwa ni
msimamo wa katiba huwezi kupinga unless uombe Constitutional amendment
kwa taratibu zilizowekwa.
So
hata kama angesema mtu mwingine ambaye si Lissu angesema kauli ileile
aliyoisema Lissu kwamba "ukifungua kesi mahakamani dhidi ya chama na
ukashindwa unakuwa umejifukuzisha uanachama mwenyewe".
Kwa
hiyo sio mawazo ya Lissu, ni msimamo wa katiba. Yani hata angesema
Mbowe, Dr.Slaa, Mnyika au mwingine yeyote angesema vilevile alivyosema
Lissu.
Wapo wanaohoji
kwanini Lissu aseme na sio Mbowe ambaye ndiye mwenyekiti? Jibu lake ni
kuwa masuala ya kisheria ndani ya chama yanaweza kusemewa na mwanasheria
wa chama. Na wanasheria wa chama ni pamoja na Lissu, John Mallya,
Mabere Marando na wengineo.
Sasa
nashangaa wanaohoji uhalali wa Lissu kuongelea msimamo wa katiba ambalo
ni jambo la kisheria. Mmesahau kuwa Lissu ni mwanasheria wa Chama? Sasa
kama mnajua Lissu ni mwanasheria wa chama mnashangaa nini anapotoa
ufafanuzi wa kisheria? Au mlitaka mambo ya sheria ayaongelee mlinzi wa
Dr.Slaa?
Wengine
wamehoji kwanini baada ya ile hukumu hakikukaa kikao kikaafikiana
kumfukuza Zitto badala ya Lissu tu kusema. Hawa ni wale ambao hawajui
hata wanachozungumza. Either ni watu wa vyama vingine so hawaijui katiba
ya CHADEMA au ni wapenzi wa chadema lakini hawapendi kusoma.
Sasa
kwa kuwasaidia ngoja niwaambie hivi. KATIBA ya CHADEMA ya mwaka 2006
inasema mwanachama yeyote atakayekipeleka chama mahakamani na akashindwa
anakua amejifukuzisha uanachama mwenyewe. Hii ina maana kuwa baada tu
ya hukumu kutoka automatically yeye sio mwanachama tena.
So bila haya Lissu kuongea lolote, Zitto alishajua yeye sio mwanachama tena. Thats legal stand.
Katiba
haikusema hukumu ikishatoka kamati kuu ikae itoe tamko NO. Katiba
inasema hukumu ikitoka kama umeshindwa kesi fungasha virago katafute
chama kingine.
Kwa
hiyo hata kama chama kisingesema lolote. Yani Lissu angekaa kimya na
viongozi wengine wote wakakaa kimya, Zitto angeondoka tu.. maana hakuna
namna nyingine. Na ungemfuata Zitto umuulize akaamua kuwa honesty
angekuambia wazi kuwa kikatiba amejifukuza uanachama mwenyewe.
Kwa
hiyo kama kuna tatizo, basi tatizo halipo kwa Lissu au Mallya au
mwanasheria yeyote wa Chadema. Kama kuna tatizo basi Tatizo lipo kwenye
Katiba ya chama.
Na
ikumbukwe wakati kipengele hicho cha katiba kinaundwa mwaka 2006 Tundu
Lissu hakuwa hata mwanachama wa CHADEMA (alikua Nccr Mageuzi), so huwezi
kuhoji legitimacy yake kwenye hicho kipengele.
Labda
ambaye anaweza kuhojiwa kwanini kipengele hicho kiliwekwa na akatoa
maelezo mazuri ni Mhe.Zitto Kabwe ambaye wakati marekebisho ya katiba
yanafanyika mwaka 2006 yeye alikuwa mjumbe wa Kamati Kuu.
Kwa
hiyo yeye ndiye anayeweza kutupa logic ya hicho kipengele. Walikiweka
ili iweje? Walimlenga nani? Kama alishiriki kuweka kipengele hicho mbona
analalamika kinapotumika kwake? Alitaka kitumike kwa nani?
Ikumbukwe
sheria ni msumeno hukata huku na huku. Unapotunga sheria yoyote jiulize
hii sheria ikitumika kwangu nitajisikiaje? Sio unatunga then ikikurudia
unahisi umeonewa.
Viongozi
wengi wa kiafrika wanapotunga sheria kandamizi (Draconian Laws) hudhani
ni kwa ajili ya tabaka la chini tu na sio kwa ajili yao. Siku
zikiwageuka wanaanza kutafuta mchawi. Katika hili Zitto hapaswi
kulalamika kabisa kuhusu kifungu cha katiba kinachomvua uanachwma maana
alishiriki kukitunga mwaka 2006.
KWANINI MDEE ANAPASWA KUJIUZULU.
Halima Mdee alitweet kile alichokiita "mawazo yake" kuwa yeye anaamini Zitto bado ni mwanachama wa CHADEMA.
Pamoja
na kuwa ni mawazo yake lakini amekosea kwa kuwa yeye kama kiongozi mkuu
ndani ya CHADEMA hakupaswa kukosoa chama chake mitandaoni. Hii ni kwa
sababu anazo platform nyingi za kukikosoa chama zaidi ya mitandaoni kama
alivyofanya.
Yeye ni
mjumbe wa Kamati kuu angeweza kuyasema huko. Yeye ni M/kiti wa BAWACHA
angeweza kuyasema huko, yeye ni mjumbe wa Baraza kuu la chama angeweza
kuyasema huko. Yeye ni mjumbe wa mkutano mkuu, angeweza kuyasemea huko.
Kwa
kifupi Mdee alikua na fursa nyingi za kusemea hayo mawazo yake badala
ya kusemea mitandaoni. Huku mitandaoni ni kwa wale wasio na fursa ya
kuwasilisha mawazo yao moja kwa moja kama ilivyo kwa Mdee. So katika
hili amekosea.
Pili,
Mdee anajua kuwa maamuzi ya Zitto kuvuliwa uanachama ni ya Katiba si ya
mtu mmoja. Si ya Lissu wala Mbowe. Ni maamuzi ya Katiba. Na Katiba hiyo
Mdee alishiriki kuitunga mwaka 2006 akiwa Mbunge viti maalum na mjumbe
wa kamati kuu. Leo anawezaje kupinga kitu kilekile alichoshiriki
kukitunga? Huu ni wendawazimu.!
Lakini
pia Mdee anajua kuwa hata kama ameona kasoro kwenye suala hili, ni
kasoro za kikatiba sio za Lissu au Mbowe. Hivyo basi mahali pazuri pa
kurekebisha kasoro hizo ni kwenye vikao vya chama si mtandaoni kama
alivyofanya. Maana hata akitweet kila siku kuwa anamtambua ZZK kuwa
mwanachama, bado Katiba iko palepale kuwa haimtambui.
Nne,
Mdee ni kiongozi wa Baraza la Wanawake na alipochaguliwa alikula kiapo
cha kuilinda Katiba ya chama. Katiba aliyoapa kuilinda ndiyo hiyohiyo
inayosema "mwanachama akikipeleka chama mahakamani akashindwa kesi
amejivua uanachama wake mwenyewe."
Sasa
mbona Mdee anapingana na katiba aliyoapa kuitetea na kuilinda? Hii ni
ajabu. Au alipoapa hakujua ndani kuna nini? Aliapa kuilinda katiba
asiyoijua? Lakini ataachaje kuijua na alishiriki kuitunga mwaka 2006?
This is paradox.!
Katika
hili Mdee kadhalilisha nafasi yake kama Mwenyekiti wa Baraza la
wanawake na mimi nashauri AJIUZULU ili kuonesha dhana ya uwajibikaji. Ni
lazima viongozi wajifunze kuwajibika kwa kauli zao.
Hatuwezi
kila siku kupigia kelele mawaziri wa serikali ya CCM wawajibike wakati
sisi wenyewe dhana ya uwajibikaji inatushinda. Kipimo kilekile
tunachowapimia CCM nasi tujipimie vivyo hivyo. Mdee achia ngazi maana
umeikana Katiba uliyoapa kuitetea.
KWANINI WENJE YUPO SAHIHI,
Ujumbe
uliosambaa ukionesha ni wa Ezekiah Wenje akichat na wabunge wenzie
kwenye group la Whatsapp juu ya sakata la Zitto nao umeibua mjadala
mkubwa kwenye jamii. Wengine wakisema ni wake wengine wakidai ni
photoshop. Na wale waliosema ni wake nao wakagawanyika. Wengine wakasema
alikua sahihi huku wengine wakiponda kuwa amekosea.
Ili
kujiridhisha kabla sijacomment kuhusu ujumbe huo nilimpigia simu Wenje
lakini hakupokea, baadae nikawapigia simu wabunge naofahamiana nao.
Wakadhibitisha kuwa ule ujumbe ni wa Wenje alioutoa kwenye group lao la
whatsapp liitwalo "CHADEMA MPs"
Baada
ya kujiridhisha kuwa ujumbe ule ni wa Wenje nikawa kwenye position
nzuri ya kuchangia, maana huwa najihadhari sana kuchangia taarifa ambayo
siielewi vya kutosha (partial informed).
So
kwa maoni yangu Wenje alikua sahihi kwa sababu alikotoa mawazo yake ni
mahali sahihi. Group ya wabunge wa CHADEMA ni sawa na kikao cha wabunge
wa chadema. So ni kikao kama vilivyo vikao vingine vya chama. Tofauti tu
ni kuwa kikao hiki kinafanyika online.
So
hiki ni kikao cha uongozi cha chama hata kama hakikua rasmi. Ndani ya
vikao kama hivi ni kawaida kuwa na mawazo tofauti baina ya wajumbe. Yani
kupingana kwa hoja lakini mwisho wa kikao wanatoka na msimamo mmoja na
msimamo huo ndio unaoenda kwa wananchi.
Sasa
Wenje ndani ya kikao kile alikua na mawazo tofauti na wenzie. Hii si
dhambi, maana ni kawaida ya vikao. Na baada ya majadiliano makali Wenje
na wengine waliokua na mtizamo tofauti wakakubaliana na maamuzi ya chama
ya kumvua uanachama Zitto maana ni ya kikatiba.
So
hadi hapo Wenje hana kosa. Kosa lipo kwa aliyevujisha taarifa hiyo ya
kikao cha ndani na kuileta public. Huyu ndiye anayepaswa kuadhibiwa.
Kuvujusha
taarifa ya vikao vya ndani ya mjumbe mwenzio kisa tu hujakubaliana nae
mawazo, ni kosa kubwa katika maadili ya uongozi.
Mbona
kuna mgogoro kwenye baraza la mawaziri na wapo ambao hawamtaki Pinda,
lakini je ni waziri gani amewahi kumrekodi mwenzie asiyekubaliana nae
mawazo na kurusha mtandaoni? Yani waziri anayemuunga mkono Pinda
akamrekodi mwenzie anayemponda Pinda kisha akarusha mtandaoni.!
Kama
hamna, sisi CHADEMA tunaojiona wakamilifu kuliko CCM hii tabia
tumeipata wapi? Mbona hao CCM tunaowakosoa kila siku wanatushinda
maadili?
Nashauri
mbunge aliyehusika "kuscreen shot" ule ujumbe wa Wenje na kuusambaza
achukuliwe hatua. Huyu hana sifa za kuwa kiongozi.
Kama
ameweza kuvujisha taarifa ya kikao cha ndani kisa tu hakubaliani na
aliyeitoa taarifa hiyo, huyu akipewa nafasi kubwa anaweza kuvujisha hata
taarifa za kuitia nchi hatarini kisa hakubaliani nayo. Narudia, mbunge
aliyehusika hafai kuwa kiongozi.!
JIPU LIMEPASUKA, SIWEZI KUWA ADUI KWA KUSEMA UKWELI.
Malisa GJ || Your Partner In Critical Thinking.!