Ofisa Miradi ya Mawasiliano, Habari na Tehama wa
Shirika la Kimataifa la Sayansi, Elimu na Utamaduni (UNESCO) nchini, Al
Amin Yusuph, akiwasilisha mada ya mchanganuo wa ufumbi wa changamoto
mbalimbali katika utekelezaji wa mradi wa kijiji cha
kidigitali.
Na
Mwandishi wetu, Bagamoyo
WADAU
mbalimbali wa elimu, afya, Tehama na masuala ya utamaduni na uchumi ambao
wamo katika mradi wa kijiji cha dijiti cha Ololosokwan kilichopo wilayani
Monduli Arusha wanakutana kwa warsha ya wiki moja ikiwa ni sehemu ya
mandalizi ya uwapo wa kijiji hicho nchini Tanzania.
Kwa
mujibu wa Ofisa Miradi ya Mawasiliano, Habari na Tehama wa Shirika la
Kimataifa la Sayansi, Elimu na Utamaduni (UNESCO) nchini Al Amin Yusuph
warsha hiyo imelenga kuangalia changamoto na namna ya kuzitatua ili mradi
kuwa na tija kwa wananchi wake.
Yusuph
alisema kwamba wadau hao wanapanga mkakati kuangalia vipaumbele na
changamoto katika utekelezaji wa mradi huo wa miaka
mitatu.
Alisisitiza kwamba kwa kuwa mradi huo utakuwa na
mawasiliano ya kisasa, masomo kwa njia ya Tehama, tiba kwa kutumia mtandao
wadau wamekusanyika mjini Bagamoyo kuangalia namna bora ya kuufanya mradi
huo uwe endelevu hata kama UNESCO na mbia wake Samsung watajiondoa huko
mbeleni.
Aliwataja baadhi ya wadau kuwa ni kutoka Wizara ya Elimu
na Mafunzo ya Ufundi, Wizara ya Afya na ustawi wa jamii, Samsung, Unesco,
wanakijiji wa Ololosokwan, waganga wa jadi wakunga, Taasisi ya elimu na
Chuo cha Ufundi cha DIT.
Alisema changamoto ambazo zinaonekana ni lazima
ziangaliwe ni pamoja na matumizi ya lugha hasa kwa kuzingatia ukweli kuwa
wengi wa wananchi wa Kimasai hawazungumzi Kiswahili
fasaha.
"tunategemea sana Tehama kufanikisha mradi huu, na lugha
inayoweza kutumiwa ni Kiswahili, sasa hili ni changamoto ni lazima
kuangalia mawasiliano" alisema Yusuph na kuongeza kuwa kuwapo kwa radio ya
jamii kutachangia kwa kiasi kikubwa kutoa nafasi ya wananchi wengi
kujifunza Kiswahili.
Aidha
alisema kwamba mambo mengine ambayo yanaangaliwa katika warsha hiyo ni
matumizi ya Tehama (intaneti) na kutoa mafunzo ya namna ya kuhudumia na
kufanyia matengenezo mitambo mbalimbali iliyomo katika mradi
huo.
Mwenyekiti wa kikundi cha elimu kutoka UNESCO, Jennifer Kotta
akishiriki kutoa maoni wakati wa warsha hiyo inayoendelea wilayani Bagamoyo
mkoa wa Pwani. Aliyesimama ni Ofisa Miradi ya Mawasiliano, Habari na Tehama
wa Shirika la Kimataifa la Sayansi, Elimu na Utamaduni (UNESCO) nchini, Al
Amin Yusuph.
Alisema nia kubwa ya kukusanya wadau mbalimbali ni
kuangalia utekelezaji wa nia ya mradi ya kuleta mabadiliko makubwa ya
kimaendeleo kwa jamii ya kimasaii ambayo kwa sasa utamaduni na uchumi wake
unatishiwa na mabadiliko ya tabia nchi.
"Tunataka maendeleo haya yasaidiwe na mawasiliano.
Tunaangalia jinsi ya kutumia mawasiliano kuleta maendeleo" alisema
Yusuph.
Alisema ni matumaini yao kwamba wabia wengine wa mradi
huu ambao ni kampuni ya simu ya Airtel watatumia uwezo wao kuhakikisha
kwamba kijiji hicho kinakuwa hewani muda wote kwa lengo la kurahisisha
huduma zinazopatikana kwa njia ya mtandao hasa tiba.
Aidha
alisema kwamba pamoja na kuleta maendeleo mradi huo unakusudiwa kuhamasisha
amani kati ya koo na makabila mbalimbali yaliyopo wilayani
Ngorongoro.
Mganga Mkuu wa wilaya ya Ngorongoro, Dkt. Peter
Kitenyi (wa kwanza kulia) akichangia maoni kwenye kikundi cha sekta ya
Afya wakati wa kutafuta suluhu ya changamoto mbalimbali zinazowakabili
jamii ya wafugaji wa kijiji cha Ololosokwan katika utekelezaji wa mradi wa
kijiji cha kidigitali huku Mwenyekiti wa kikundi hicho kutoka UNESCO, Bw.
Mathias Herman(katikati kulia) akiorodhesha maboresho ya changamoto
hizo.
Katika
warsha hiyo ambapo wadau wamegawanyika makundi mbalimbali ili kutengeneza
hoja za kufanyia kazi kwa ajili ya kufanikisha masuala ya elimu na
afya.
Katika
elimu wameangalia vikwazo ikiwa ni pamoja na ndoa za utotoni na watoto
kuacha shule kwenda kuchunga mifugo.
Ili
kukabiliana na kiwango kikubwa cha kutojua kusoma na kuandika kipaumbele
kinachofikiriwa ni kuwafikia vijana hao wakiwa machungani kwa kuwapelekea
mafunzo kwa njia ya mtandao.
Afisa
Mipango wa Elimu wa Unesco, Jennifer Kotta alisema changamoto ya elimu
katika kijiji hicho na majirani ni kubwa na kwamba wanachofikiria ni
kutumia Tehama ambapo sasa watawafikia vijana kule
waliko.
Wadau mbalimbali wa Elimu, Afya, Tehama na masuala ya
utamaduni na uchumi wanaoshiriki warsha ya wiki moja inayofanyika wilayani
Bagamoyo mkoa wa Pwani ikiwa ni sehemu ya mandalizi ya uwapo wa kijiji cha
dijiti cha Samsung cha Ololosokwan kilichopo wilayani Ngorongoro mkoani
Arusha.
Aidha
wamepanga kufunza lugha ya Kiswahili na Kiingereza ili kutanua wigo wa
majadiliano wa wakazi wa eneo hilo na watalii wanaofika na kupenda kununua
kazi zao.
Warsha
hiyo iliyofunguliwa na Mkurugenzi Mkazi wa Unesco nchini inafanyika wakati
vifaa vya kutengeneza kijiji hicho vikiwa vimeshaondoka katika bandari ya
Dar es salaam.
Katika
masuala ya Afya wadau wameangalia vipaumbele vinavyostahili sasa ikiwa ni
pamoja na utunzaji wa mimba na mtoto.
Wamesema wanawake wa kimasai wanafanya shughuli nyingi
kuanzia ujenzi wa makazi na ukamuaji wa maziwa hadi ulezi wa watoto na
kusema katika mazingira hayo wanahitaji sana elimu ya uzazi
salama.
Mwenyekiti wa kikundi cha Sanaa na ubunifu kutoka
UNESCO, Courtney Ivins (wa pili kushoto) wakijadiliana na wanakikundu
wenzake kuhusu changamoto mbalimbali zinazoikabili sekta ya utamaduni
hususani kwa wakimama wa kimasai wanaotengeneza bidhaa za shanga jinsi ya
kuziboresha na kuvutia watalii wanaotembelea hifadhi ya Ngorongoro mpaka
kijiji cha Ololosokwan pamoja na jinsi ya kutatua migogoro ya ardhi iliyopo
kwenye jamii za wafugaji.
Ofisa Miradi ya Mawasiliano, Habari na Tehama wa
Shirika la Kimataifa la Sayansi, Elimu na Utamaduni (UNESCO) nchini, Al
Amin Yusuph (wa kwanza kulia) wakiwa kwenye majadiliano na kikundi chake
huku wakiangalia changamoto mbalimbali za masuala ya Tehama zinazoikabili
kijiji cha Ololosokwan kwa ajili ya kuziboresha ikiwa ni maandalizi ya
kupokea mradi wa kijiji cha kidigitali.
Mwenyekiti wa kikundi cha elimu kutoka UNESCO,
Jennifer Kotta (wa tatu kushoto), Mkurugenzi wa elimu ya msingi kutoka
Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Sarah Mlaki (wa kwanza kushoto) na
wadau kutoka Ololosokwan wakianisha changamoto na utatuzi wa changamoto
kwenye sekta ya elimu katika kuboresha utekelezaji wa mradi wa kijiji cha
kidigiti cha Samsung cha Ololosokwan wakati wa warsha ya wiki moja
iliyoandaliwa na UNESCO wilayani Bagamoyo mkoani
Pwani.
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia