TAHARIRI: JUHUDI HIZI ZA WAZIRI MKUU PINDA KUSAIDIA SHULE ALIYOSOMEA ZIUNGWE MKONO

photo 4
Pichani juu na chini ni baadhi ya majengo yaliyokamilika ya Shule ya msingi Kakuni yaliyojengwa na Waziri Mkuu Pinda kupitia michango ya wadau wa maendeleo.
Na Andrew Chale 
Kila mmoja wetu anatambua mchango mkubwa wa elimu hasa ile inayotolewa ikiwemo ngazi ya Awali, Msingi, Sekondari na elimu ya juu ikiwemo chuo. Pia katika hilo ni jamb la msingi sana na la maana hasa unapokumbuka mahala ulipopatia elimu husika.
Mtandao  wa Mo dewjii blog tunapenda kuungana na kumpongeza Waziri Mkuu, Mizengo Pinda kwa juhudi zake za dhati kabisa katika kuhakikisha shule yake aliyowahi kusoma hapo inasaidiwa na kufikia malengo yake.
Waziri Mkuu alipaata elimu yake katika Shule ya msingi Kakuni. Kwa kusoma hapo darasa la kwanza hadi la nne. Lakini kwa mapenzi mema na juhudi za kutaka kuona watoto wa hali ya chini hasa wa wakulima wanapata elimu bora, kwa juhudi zake binafsi, ameweza kusaidia shule hiyo ikiwemo kutafuta wafadhili mbalimbali wa kuipiga tafu, akiwa kama Mizengo Pinda. Ambapo unaweza kusoma kiunganishi hichi hapa cha mtandao ili kusoma habari hiyo zaidi ya wadau kumuunga Waziri Mkuu Pinda katika kuisaidia shule ya Kakuni: http://dewjiblog.com/2015/03/11/japan-yachangia-sh-milioni-160-shule-ya-msingi-kakuni/
photo 1
Mtandao huu unapongeza juhudi hizo za Waziri Mkuu Mizengo Pinda hivyo pia nawe ukiwa ni miongoni mwa unayeguswa na maendeleo ya elimu hapa nchini, ni wakati wa kutembelea shule yako uliosoma awali iwe elimu ya ‘vidudu’ yaani Chekechea/Awali, Shule ya Msingi ama Sekondari basi ni wakati wa kurejea na kusaidia chochote kile ili kuendeleza Elimu hapa Nchini.
Bila shaka kama Watanzania tutaiga juhudi hizi za Waziri Mkuu Mizengo Pinda, bila shaka elimu ya Tanzania itapanda maradufu kwani tumeweza kushuhudia kwa upande wa juhudi hizo za Mizengo Pinda ikiwemo kushawishi wadau ikiwemo Serikali ya Japan, kutoa msaada wa dola za Marekani, 90,286, ambazo ni sawa na Sh. Milioni 160.
Fedha hizo ni kwa ajili ya kusaidia ujenzi wa Shule ya Awali kwenye Shule ya Msingi, Kakuni iliyopo kijiji cha Kibaoni, Wilaya ya Mlele, Mkoa wa Katavi.
PM-PINDA
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Mizengo Pinda.
Juhudi za Mizengo Pinda za kuanzisha wazo hilo la kusaidia kuijenga shule yake ni kama njia ya kumshukuru Mungu na kuwashukuru wananchi waliosaidia kumfikisha hapo alipo.
Kwani alipata kusoma darasa la kwanza hadi la nne katika shule ya msingi Kakuni mwaka 1957 hadi 1960.
Hivyo, tunatambua wapo wasomi wengi, wapo wabunge, wapo Mawaziri, wapo Wakurugenzi na wengine wenye vyeo vikubwa Serikali, sekta binafsi na waliopo ndani nje ya nchi, shime tujitokeze kwa wingi kwa kila mmoja kwenda kwenye shule aliyosoma na kuchangia chochote.
Tunatambua sisi tumepata elimu wakati gani na kiwango cha elimu wakati huo kilikuwaje, hivyo tutakapojitokeza kama alivyofanya Waziri Mkuu Mizengo Pinda, hii itasaidia kukuza elimu yetu hapa Nchini.
photo 3
Muonekano wa majengo yaliyokamili ya shule ya msingi Kakuni alipopata elimu ya msingi Waziri Mkuu Pinda na kuamua kuijenga upya kwa gharama ya zaidi ya Shilingi bilioni 1.3/- kutokana na michango ya wadau mbalimbali wa maendeleo.
photo 5

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

Previous Post Next Post