Bingwa
wa mbio ndefu za kilomita 42 za Kilimanjaro Full Marathon, Fabiola
Willium akimaliza mbio hizo katika mashindano ya mbio za Kilimanjaro
Marathon zilizofanyika Moshi
Mshindi
wa mbio ndefu za Kilomita 42 za Kilimanjaro Full Marathon, David Ruto
akimaliza mbio hizo katika mashindano yalika Moshi leo
Washiriki
wa mbio fupi za Kilomita 21 za Tigo Half Kili Marathon wakichuana
wakati wa mashindano ya mbio za Kilimanjaro Marathon 2015 zilizofanyika
Moshi
**************
Mwana dada wa Tanzania Fabiola William
(32),ameibuka mshindi wa kilomita 42 (Full Marathon woman) katika mbio za
Kilimanjaro Marathon zilizofanyika leo katika viunga vya mji wa Moshi mkoani
Kilimanjaro.
Fabiola ametumia muda wa saa 2:49:51 na
kujinyakulia kitita cha shilingi milioni 4 kutoka kwa wadhamini Kilimanjaro
Lager na kuwaburuza wakenya Rosaline David, Joan Cherop, Dorice Todipus, Sarah
Maiyo , Gladys Cheruiyo , Susan Koskei, Julitter Tanin, Esther Mutuku na Lilian
Chelimo walioshika namba 2 hadi 10.
Full Marathon wanaume, David Ruto
(Kenya), aliibukamshindi baada ya kutumia 2:15:50 na kuzawadiwa Sh milioni 4
huku nafasi ya pili hadi ya tano zikienda Kenya kwa wakimbiaji, Benard Kimayo, Alex
Bartida, George Ngure na Douglas Chebii.
Mtanzania Pascal Mombo alijitokeza na
kushika nafasi ya sita huku wakenya David Kilimo, Lawrence Rotich, Mathew
Koskei wakichukuanafasi ya 7 hadi 9 na Mtanzania Siegried Ngolly kumaliza wa
kumi.
Aidha katika mbio za Kilomita 21,
nafasi ya kwanza hadi ya nne ilikwenda kwa Watanzania, Ismail Juma, Emmanuel Giniki, Theotil Joseph,
Felix Alfonse huku nafasi tano hadi ya nane ikienda Kenya kupitia Festus Stalamestus, Vicent Kipruto, Fanuel
Mkungo na Dickson Kimuthi, Mtanzania Elia Sidame alimaliza wa tisa na mkenya
Martin Muhinde kumaliza wa kumi.
Upande
wa wanawake Half Marathon Kilomita 21, wakim,biaji wa Kenya walifanya vyema kwa
kuchukua tano bora ikiongozwa na Grace Kimanzi ,Yunice Echumba, Vicoty
Cherkemai, Sherekith Nyawera, Jane Mwikal.
Nafasi
ya sita hadi ya nane ilikwenda kwa watanzania Failuna Abdi, Mary Naali na Catherine Lange na
tisa na kumi zikenda Kenya Yunice Mutie na
Ludera Fida.
Akizungumza katika mbio hizo, mgeni rasmi Waziri wa Mambo ya Ndani, Mathias Chikawe, alisema aliwapongeza waandaaji wa tukio hilo la aina yake.
“Nawapongeza sana wadhamini wakuu Kilimanjaro Premium Lager, waandaaji na wadau mbalimbali ambao kwa pamoja mmefanikisha mbio hizi kwa miaka 13 sasa,” alisema.
Pia aliwapongeza GAPCO kwa kudhamini mbio za walemavu pamoja na wadhamini wengine ikiwemo Grand Malt, Simba Cement, KK Security, Keys Hotel, TPC Sugar, CMC Automobiles Ltd, RwandAir, FNB Tanzania, Kibo Palace Hotel, UNFPA, Kilimanjaro Water, pamoja na wadhamini shirikishi wapya kabisa katika mbio hizi ambao ni NSSF na Tanzania Coffee Board.