KAMANDA WA UVCCM ,ACHANGISHA MILIONI 30 SUYE

KAMANDA wa umoja wa vijana wa ccm mkoa wa Arusha(UVCCM)Philemon Mollel
ameongoza harambee ya kuchangia ujenzi wa ukuta wa shule na choo
katika shule ya sekondari Suye ya jijini hapa na kufanikisha
kupatikana kiasi cha zaidi  ya sh,milioni 38.

Harambee hiyo iliyofanyika jana shuleni hapo,ililenga kupatikana kwa

shilingi milioni 60,fedha ambazo zingetosha kumaliza changamoto
mbalimbali baada ya kubadili majengo yaliyokuwa yakitumika kama
kiwanda .

Kabla ya harambee hiyo Mollel ambaye alikuwa mgeni maalumu,aliahidi

kushughulikia suala la upungufu wa walimu wa masomo ya sayansi na
Hisabati katika shule hiyo.

Aliwataka wazazi waache tabia ya utegemezi pekee kwa kutegemea

serikali iwaletee maendeleo bali aliwasihi wajiwekee utaratibu wa
kuchangia maendeleo ya shule ,jambo ambalo litaongoza weredi wa masomo
katika shule hiyo.

''Bila mipango hakuna mafanikio wazazi wachukulie uchangiaji wa

maendeleo ya elimu kama sehemu ya maisha yao kwa kujinyima kidogo
wanachopata ,sual hilo ni jema sana ,lakini tukitegemea kila kitu
serikali tutabaki nyuma  kila siku,  hakuna mbadala wa elimu.''alisema
Molel.

Naye mkuu wa wilaya ya Monduli Jowika Kasunga aliyemwakilisha mkuu wa

mkoa wa Arusha,Felix Ntibenda aliishukuru halimashauri ya jiji kwa
kukubali kubadilisha kiwanda hicho kichokuwa kimekuwa kuwa shule ya
sekondari.

Alisema kuwa hali hiyo itasaidai sana kuwapatie elimu vijana wa eneo

hilo ambao awali walitumia muda mwingi kufuata elimu ya sekondari
kutokana na umbali wa eneo hilo.

''Hili eneo lilikuwa  dangulo kwa miaka mingi haya majengo yalipaki

kama gofu na kutumiwa kama maficho ya wahalifu lakini sasa
pamebadilika na kupendeza sana,wazazi itumieni shule hii vizuri
''alisema Kaasunga.

Awali mkuu wa shule hiyo Sarah Milunga alisema shule hiyo inajumla ya

wanafunzi wa 800 na kwamba inakabiliwa na changamoto nyingi ikiwemo ya
uhaba wa walimu,aliwaomba wahisani ,mashirika mbalimbali ,watu binafsi
na makampuni kuona umuhimu wa kuisaidia shule hiyo changa .

Katika harambee hiyo jumla ya shilingi milioni 38,717,500 zilipatikana

zikiwemo fedha tasilimu sh,milioni 24,027,500 ahadi ni sh,milioni
14,690,000 pamoja na mifuko 120 ya simenti.Hata hivyo Mollel
akichangia sh,milioni 10,RC Ntibenda 500,000 na halmashauri ya jiji
kupitia afisa elimu sh,milioni 9.

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

Previous Post Next Post