Mwanadada
Chiku Ketto a.k.a Chiku K Balaa ameamua kuweka wazi hisia zake
alizonazo kuhusu kile anachokiona kinamtesa Aliyekuwa Member Mwenzake wa
Kundi la LaFamilia.
Akizungumza
na Kipindi cha DUNDO cha MamboJambo Radio Arusha kupitia Kipengele cha
DROP BOX Chiku amesema ana mpango wa kukaa Karibu zaidi na Chid Beenz
Kwakuwa anajua anakoelekea sio kwema kwani wakati wakiwa Pamoja Chid
alikuwa na Mafanikio na Hakuwa kama alivyokuwa Kitu ambacho kinaonekana
kama Chid beenz amekosa mtu wakuwa karibu zaidi na yeye kwa Ushauri na
Ukaribu wa Kimawazo Chanya.
Bila
shaka mmefuatilia pia Kesi ambayo ilikuwa inamkabili Chid Beenz ambayo
ilikuwa ya Kukutwa na Madawa ya Kulevya Katika Uwanja wa JK Nyerere
Airport na kuachiwa huru kwa Faini ya sh. 900 000/= za Kitanzania Hivi
juzi hii ni moja ya sababu zinazoonyesha Chid Baanz amefikia kubaya
zaidi.
UKIWA
unakumbukumbu nzuri sana utakumbuka wakati ule chid akiwa na LaFamilia
Team yake hata kiafya alikuwa Kajaza na hata watu walikuwa wanamuogopa
kwa kuwa alikuwa na Lile Body Flani la Kinako ila kwa sasa hata machalii
wanweza kumchezea Japo Wembamba hauna maana ya kuwa Umeisha na nguvu
ila kiukweli Chid Amepungua sana Kiafya.
- CHID BEENZ ENZI HIZO
Chiku
amemshauri Chid Kuhakikisha Anakumbuka kuna Mama yake, Ndugu zake
Wanamtegemea na pia Jamii nzima inamwangalia na Cha Mwisho akasema
anampenda sana Chid Beenz Kuna ngoma wamefanya kwa Pamoja na
Atahakikisha Kuwa Chid anaepukana na Majanga yanayomwandama.
Katika
Mazungumzo hayo Chiku amepata Pia nafasi ya Kuzungumzia Ngoma zake
Mbili ambazo zinatoka mwisho wa Mwezi huu au mwanzoni mwa mwezi ujao
Ambapo ngoma hizo mojawapo ni PIGA HATUA ambayo ilikuwa itoke mwaka jana
Mwishoni lakini ikashindwa kutoka sababu alizozitaja kuwa ni Matatizo
yaliyokuwa yametokea katika Management yake na Ya Pili ni ngoma ambayo
itakuwa inahamasisha Vijana Kupiga Kura Ukizingatia huu ni mwaka Muafaka
kwa Watanzania Kumchagua Rais Mpya, Wabunge na Madiwani katika Serikali
Kuu ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania.
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia