Diwani Viti maalum Bi.Kezia Magoko akitilia mkazo kuwa Waziri Mkuu mstaafu na Mbunge wa Monduli Edward Lowassa ni chaguo la wengi
Mjumbe
wa halmashauri kuu ya chama cha mapinduzi wilaya ya Serengeti Daniel
Kegocha ambaye pia ni diwani aliomba chama hicho kuona umuhimu wa
kumpitisha jina la Waziri Mkuu mstaafu na Mbunge wa Monduli Edward Lowassa kwa kuwa ni chaguo la walio wengi na yeyote anayetokea kupinga atakuwa ni msaliti katika chama hicho.
Wadau wakifwatilia mkutano wao na wanahabari
WANANCHI wa wilaya ya Serengeti mkoani Mara wamekitaka chama cha mapiduzi (CCM) kutokuzuia demokrasia ya wanachama kushawishi wagombea wa uraisi wanaona kuwa wanafaa kuwatetea kiti cha uraisi.
Wakizungumza
jana mkoani hapa,baada ya kufika nyumbani kwake kwa lengo la
kumshawishi Waziri Mkuu mstaafu na Mbunge wa Monduli Edward Lowassa
kugombea nafasi ya uraisi ,wananchi hao walisema kuwa ni vyema chama
kikawaacha wapenzi na mashabiki wa Lowassa kuendelea kumshawishi
agombee na nafasi hiyo.
Akizungumza
na waandishi wa habari aliyekuwa katibu wa umoja wa wanawake wa {UWT}
chama cha mapinduzi wilaya ya Serengeti Anna Mathayo Chacha alisema kuwa
lowasa ndie chaguo lao kwa kuwa ni kiongoziwanayeamini kuwa ataivusha
nchi kutoka hapa ilipo ikiwa ni pamoja na kukipa heshima na nguvu
chama.
Aidha
alisema kuwa wananchi wanahitaji utawala bora kwa sasa na mtu pekee
ambaye wanadhani anatosha nafasi hiyo ni Edward Lowassa kwa kuwa ni
kiongozi mwenye maamuzi magumu ambaye anaweza kusimamia utawala bora
hivyo viongozi wa ngazi za juu wasizue demeokrasia ya wananchi kusema
ambacho wanahisi ni sahihi kwao.
Diwani
wa kata ya Ikoma Sebastian Sabasaba Banagi alisema kuwa sauti ya wengi
ni sauti ya Mungu hivyo kitendo cha kuzuiwa kwa wananchi kueleza hisia
zao sio jambo la kidemokrasia bali linakandamiza uhuru wa kusema
wanachokiamini.
Alisema
kuwa ili suluhu ya chama cha mapinduzi kushinda katika uchaguzi mkuu ni
kumpitisha Lowassa kwa kuwa wao kama viongozin ambao wanawawakilisha
wananchi na wananchi wanapendekeza kiongozi huyo kuwania kiti hcho
kutokana na matumaini na imani kubwa walioyo nayo kwake.
“kama
alivyosema Waziri mkuu mstaafu ,Lowassa kuwa huwezi kuzuia mafuriko kwa
mikono ni sahihi kabisa hata sisi tunaliunga mkono hilo hakuna mtu
yeyote anayeweza kuzuia hisia za watu juu ya kiongozi huyu
mahiri”alisema Banagi
Kwa
upande wake mjumbe wa halmashauri kuu wa chama cha mapinduzi wilaya ya
Serengeti Daniel Kegocha aliomba chama hicho kuona umuhimu wa kumpitisha
jina la mgombea huyo kwa kuwa ni chaguo la walio wengi na yeyote
anayetokea kupinga atakuwa ni msaliti katika chama hicho.
Alisema
kuwa, ni vizuri kamati kuu ya chama kukaa chini kwa pamoja kutafakari
na kuona umuhimu mkubwa wa kumpitisha mgombea huyo kwa kuwa kila kona
ya nchi wana imani naye na wana amani atawaletea maendeleo na
kuliunganisha Taifa.
Wanachi
hao kutoka wilayani Serengeti wakiongozwa na madiwani ,wananchi wa
kawaida na waiowahi kushika nyadhifa katika chama hicho wapatao 65
wamefika wilayani Monduli ili kumshawishi mbunge huyo kutokata tamaa na
kuendelea na nia ya kuchukua fomu huku wakiahidi kuwa ni watamfuata
alipo ili kumshawishi na kuzungumza nae.