BREAKING NEWS

Monday, March 30, 2015

TASWIRA YA MATEMBEZI YA HAMASA KUPIGA VITA MAUAJI YA ALBINO - IMETOSHA


Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe na Mbunge wa Viti Maalum, Al Shaymar Kweigyr wakiongoza matembezi ya hamasa ya kupiga vita mauaji ya albino nchini yaliyofanyika leo jijini Dar es salaam kuanzia viwanja vya Biafra mpaka Leaders Club, Kinondoni jijini Dar es salaam.
Matembezi yakiendelea.

Wadau kutoka sekta mbali mbali wakishiriki kwenye Matembezi ya hamasa ya kupiga vita mauaji ya albino nchini yaliyofanyika leo jijini Dar es salaam kuanzia viwanja vya Biafra mpaka Leaders Club, Kinondoni jijini Dar es salaam.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe, Mbunge wa Viti Maalum, Al Shaymar Kweigyr, Balozi wa Harakati ya Imetosha, Henry Mdimu, Mwakilishi wa Chama cha Albino Tanzania (TAS), Abdillah Omar sambamaba na wadau wengine wakishiriki kuimba wimbo 'Tanzania Tanzania' kabla ya kuanza kwa shughuli nzima ya hamasa ya kupiga vita mauaji ya albino nchini, iliyofanyika leo kwenye viwanja vya Leaders Club, jijini Dar es salaam.


Mbunge wa Viti Maalum, Al Shaymar Kweigyr akicheza muziki wa sambamba na Mwanamuziki wa Reggae,Jhiko Manyika "Jhikoman" wakati wa shughuli nzima ya hamasa ya kupiga vita mauaji ya albino nchini, iliyofanyika leo kwenye viwanja vya Leaders Club, jijini Dar es salaam.Kulia ni Mwenyekiti wa Tanzania Bloggers Network ambao ni wadau wakubwa wa harakati ya Imetosha, Joachim Mushi.
Mwanamuziki wa Reggae,Jhiko Manyika "Jhikoman" (katikati) akizungumza machache ikiwa ni sehemu ya hamasa ya kupiga vita mauaji ya albino nchini, iliyofanyika leo kwenye viwanja vya Leaders Club, jijini Dar es salaam.Kushoto kwake ni Mbunge wa Viti Maalum, Al Shaymar Kweigyr na kulia kwake ni Balozi wa Harakati ya Imetosha, Henry Mdimu pamoja na Mwakilishi wa Chama cha Albino Tanzania (TAS), Abdillah Omar.Kulia ni Mwenyekiti wa Tanzania Bloggers Network ambao ni wadau wakubwa wa harakati ya Imetosha, Joachim Mushi.
"Selfie" Sehemu ya wajumbe wa Kamati ya Imetosha wakiwapa picha ya pamoja.
Mdau Rama na Dada Salma.
Mdau Mkala Fundikira akitafuta taswira.
MC Mzee Mdachi akiwajibika leo.
Mwenyekiti wa Tanzania Bloggers Network ambao ni wadau wakubwa wa harakati ya Imetosha, Joachim Mushi akizungumza machache kwa niaba ya Wanablog wote Tanzania.
Mgeni Rasmi,Mh. Mathias Chikawe akiwa kwenye shughuli hiyo.
Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Matembezi ya Hamasa ya kupiga vita mauaji ya albino nchini (Imetosha), Ally Masoud "Kipanya" akiwa na Mmoja wajumbe wa Kamati yake,Monica Joseph.
Wadau.
Dada Victoria.

Doris Molel wa Doris Molel Foundation akifatilia hotuba ya Mgeni Rasmi.
Mgeni Rasmi.
Mwakilishi wa Chama cha Albino Tanzania (TAS), Abdillah Omar.
Dada Neema wa Kamati ya Imetosha.
Wadau wa Kamati ya Imetosha.
Rais wa Shirikisho la Filamu Tanzania (TAFF),Simon Mwakifwamba akizungumza machache.

Balozi wa Harakati ya Imetosha, Henry Mdimu akiwa na rafiki yake wa kitambo na Msanii wa Kuigiza,Isaya Mwakilasa "Wakuvanga" pamoja na mwanae.



Doris Molel na rafiki yake ambao kwa pamoja wameanzisha Doris Molel Foundation maalum kwa kusaidia watoto wanaozaliwa kabla ya muda (Njiti) wakizungumza kwenye shughuli ya hamasa ya kupiga vita mauaji ya albino nchini, iliyofanyika leo kwenye viwanja vya Leaders Club, jijini Dar es salaam.

Wajumbe wa Kamati ya Imetosha, Kelvina John (kulia) na Neema Lissa 
Mkongwe katika yasnia ya Muziki nchini,John Kitime akiimba wimbo maalum wa hamasa ya kupiga vita mauaji ya albino nchini, iliyofanyika leo kwenye viwanja vya Leaders Club, jijini Dar es salaam.
Mwanamuziki Vital Maembe akiimba wimbo maalum wa hamasa ya kupiga vita mauaji ya albino nchini, iliyofanyika leo kwenye viwanja vya Leaders Club, jijini Dar es salaam.
Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Matembezi ya Hamasa ya kupiga vita mauaji ya albino nchini (Imetosha), Ally Masoud "Kipanya" akizungumza kabla ya kumkaribisha Balozi wa Harakati ya Imetosha, Henry Mdimu ili kuzungumza na Watanzania waliofika kwenye Viwanja vya Leaders Club, Kinondoni jijini Dar es salaam leo.
Wawakamati wa Imetosha na Balozi wa Imetosha.
Mwanahabari akirekodi tukio zima la Imetosha.
Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Matembezi ya Hamasa ya kupiga vita mauaji ya albino nchini (Imetosha), Ally Masoud "Kipanya" akimkaribisha Balozi wa Harakati ya Imetosha, Henry Mdimu ili kuzungumza na Watanzania waliofika kwenye Viwanja vya Leaders Club, Kinondoni jijini Dar es salaam leo.
Msanii Cassim Mganga na Fundikira.
Wadau.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mh. Mathias Chikawe akitoa hotuba yake na kauli ya Serikali katika harakati ya kupambana na kupiga vita mauaji ya albino nchini, iliyofanyika leo kwenye viwanja vya Leaders Club, jijini Dar es salaam leo.
 Wadau wakiburudika.



Share this:

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

 
Back To Top
Copyright © 2014 MOUNT KILI NEWS. Designed by OddThemes | Distributed By Gooyaabi Templates