Ikiwa ni baada ya tamko la Kinabii
juu ya mwaka 2015 kuwa ni mwaka wenye meno na unang’ata kwa waganga wa
kienyeji,washirikina na wachawi.Hatimaye
JESHI la Polis mkoani Kagera limeanza
opereisheni ya kuwasaka waganga na wapiga ramli,ikiwa ni harakati za kutokomeza
vitendo vya mauaji vinavyodaiwa kusababishwa na baadhi ya waganga wa kienyeji
kwa kutoa ushauri kwa waharifu.
Opereisheni hiyo endelevu imeanza
Machi 4 kwa kuwahusisha katika wilaya ya Biharamulo kwa kuwashirikisha
askari Polis pamoja na kikosi cha Mali Asili,nakufanikiwa kuwakamata jumla ya
wapiga ramli 18 waliokuwa katika viji vya kata nne za Kabindi,Nyamigogo,Runazi
na Nyabizozi zote zikiwa ndani ya tarafa Nyarubunga wilayani Biharamulo.
Kamanda wa jeshi la Polis mkoani
hapa Hennry Mwaibambe,akiongea katika tukio hilo katika kituo cha Polis
Kabindi,Opereisheni hiyo imeanza ili kuhakikisha vitendo vya mauaji na
kishirikina vinatokomezwa,kwani vitendo vya mauaji vimekuwa vikishamiri katika
maeneo ya wilaya ya Biharamulo.
Kamanda Mwaibambe alisititiza kuwa
opereisheni hiyo si nguvu ya soda,bali itakuwa endelevu kwani wapo baadhi ya
wahusika na vitendo vya uharifu wa mauaji wamekuwa wakihusika katika mauaji ya
binadamu kwa kutafuta viungo vya binadamu hasa kwa kuwaua binadamu wenye
ulemavu wa ngozi(Albino) hivyo jeshi la Polis mkoani Kagera kwa kushirikiana na
maafisa wanyama poli poli la Burigi,watahakikisha wanapambana na hali
hiyo.
"Jeshi letu limejipanga
kuhakikisha linalinda watu hawa(wenye ulemavu wa ngozi)tunaomba jamii iwe
tayari kuwafichua wale wote wenye dhamira na kujihusisha katika vitendo hivyo
vya kijama,vitendo hivi vinalitia doa taifa letu,lazima tuhakikishe
tunatokomeza hali hii!natoa onyo kwa wale wanajihusisha na shughuli ya upigaji
ramli na uganga wa kienyeji.tabia hii haivumiliki tena!"alisisitiza Kamanda
Mwaibambe.
Aliongeza mara baada ya kukamilika
taratibu za mahojiano,watuhumiwa wote 18 waliokamatwa watafikishwa mahakamani
ili kujibu mashitaka yaliyo mbele yao.
chanzo :N.Y.U radio
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia