MBUNGE AWAMWAGIA WAMAMA MAMILIONI YA FEDHA

MBUNGE wa viti maalumu ,Joyce Mukya kupitia taasisi yake ya Joy
Foundational ameanzisha mpango wa kuwakwamua kiuchumi wanawake wa jiji
la Arusha kwa kuwapatia msaada wa fedha kupitia vikundi vyao vya
ujasiriamali watakazo zitumia kukopeshana.

Akizungumza na gazeti hili wakati akikabidhi fedha tasilimu kwa akina

mama waliopo katika kata za Sakina,Sombetini na Engutoto jijini
Arusha,alisema msaada huo utawasaidia wakina mama kujiajiri wenyewe
kwa kufanya biashara ndogo ndogo na kwamba hata hitaji kureejeshewa
fedha hizo .

Alisema anajisikia uchungu kuona mwanamke akiteseka kutokana na

majukumu mengi ikiwemo kulea na kusomesha watoto huku waume zao
wakiendekeza starehe za unywaji wa pombe bila kujali famila zao.

Alisema hali hiyo ndio imemsukuma na kuamua kutenga zaidi ya shilingi

milioni 20 na kuzigawa kama msaada kwa wanawake watakao kuwa
wamejiunga kwenye vikundi katika kata zote 28 za jijini Arusha.

''Nimeamua kutoa mchango wangu kwa wanawake kama sehemu ya majukumu

yangu kama mama nina mtoto ninaleaa najua shida za mwanamke ,hizi
fedha sio kwamba sizihitaji ila lengo langu ni kumkwamua mwanamke
mwenye uhitaji''alisema Nkya.

Aidha alisema tayari ameshatoa kiasi cha shilingi milioni 6.5 katika

kata nne za jiji la Arusha ,ambapo kata ya Moshono aliwapatia kikundi
cha akina mama shilingi milioni 1.5 kati ya million 3 alizoahidi,kata
mpya ya Sakina sh, milioni 1.5,kata ya Sombetini sh,milioni 2 na kata
ya Engutoto sh,milioni 1.5.

Alisema lengo lake ni kuona fedha hizo zikistawi na kuwanufaisha

wanawake wengi zaidi jijiji haapa na baadae kuongeza zaidi mfuko wao
ili kupanua wigo wa kukopeshana

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

Previous Post Next Post