Rais
Jakaya Mrisho Kikwete na mkewe Mama Salma wakitoa heshima za mwisho
kwa mwili wa marehemu Kapteni John Komba mbunge wa jimbo la Mbinga
Magharibi katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam leo.Kapteni
Komba anatarajiwa kuzikwa kijijini Kwake Lituhi wilaya ya Nyasa Mkoani
Ruvuma.
Rais
Jakaya Mrisho Kikwete na mkewe Mama Salma Kikwete wakimfariji mjane wa
marehemu Salome Komba katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam
leo
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, wakeze
Mama Zakhia Bilal na Mama Asha Bilal, wakitoa heshima zao za mwisho mbele ya
jeneza lenye mwili wa marehemu, Kapteni John Komba, wakati wa shughuli za kuaga
mwili huo zilizofanyika leo Machi 2, 2015 kwenye Viwanja vya Karimjee jijini
Dar es Salaam. Baada ya shughuli hiyo mwili wa marehemu umesafirishwa kuelekea Kijiji
cha Litui Wilayani Mbinga mkoa wa Ruvuma kwa maziko.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akisalimiana na Waziri Mkuu Mstaafu, Edward Lowassa, wakati walipokutana kwenye
Viwanja vya Karimjee baada ya kuhudhuria shughuli za kuaga mwili wa marehemu
Kapteni John Komba leo Machi 2, 2015. Baada ya shughuli hiyo mwili wa marehemu
umesafirishwa kuelekea Jijini cha Litui Wilayani Mbinga mkoa wa Ruvuma kwa
maziko.