Mwenyekiti wa Unity Women Foundation
(UWF), Maryam Ajmy akiwa akikusanya misaada waliyokuwa wakitoa katika
hospitali ya Ocean Road jijini Dar es Salaam kutoa msaada kwa wanawake
ikiwa ni kuadhimisha siku ya wanawake duniani iliyofanyika hivi
karibuni.
Mwenyekiti wa Unity Women Foundation (UWF),
Maryam Ajmy akiwa na wanaumoja wenzake wakiingia hospitali ya Ocean
Road jijini Dar es Salaam kutoa msaada kwa wanawake ikiwa ni
kuadhimisha siku ya wanawake duniani iliyofanyika hivi karibuni.
---
Chalila Kibuda, Globu ya
Jamii.
Unity Women Foundation (UWF), umetoa msaada kwa
wanawake wagonjwa katika hospitali ya Ocean Road jijini Dar es
Salaam.
Akizungumza na baada ya kutoa msaada katika Siku
ya Wanawake Duniani iliyofanyika hivi karibuni, Mwenyekiti wa UWF, Mariam
Shamo amesema wanawake wanatakiwa kujitoa kwa wanawake wenzao wenye
matatizo kwa siku zote kutokana na kuwepo kwa wanawake wengine hawana
msaada wa mtu yeyote.
Mariam amesema wanawake siku ya wanawake itumike
kwa kwa kufariajiana na kuendelea na kuweza kuona kuona mabadiliko na
kuweza kutatua changamoto zetu zinazotukabiri.Amesema wanawake wenye uwezo
wasaidie na kuwatembelea wanawake wenzao katika wodi mbalimbali na kutoa
msaada hata kama ni kidogo lakini kinathamani yake.
Aidha amesema kama UWF wataendelea kutoa
kuwafariji wagonjwa kila muda ili nao waweze kujua wanawake wa nje yao
wanatambua matatizo yao.