Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue (kushoto)
akimsikiliza Mshauri Mkuu na Mlezi wa Ikulu SACCOS Bw Joseph
Sanga (wa pili kulia) akimuelezea mikakati ya ushirika huo
wakati wa hafla fupi ya kumkabidhi kitabu chake cha
uanachama wa ushirika huo Ikulu Dar es salaam. Wa pili
kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa Ikulu SACCOS, Bw. Deodatus
Gaudio, akifuatiwa na Katibu wake Bw. Benedicto Damiano na
kulia ni Mtunza Hazina Bi. Judith Medson.

Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue akipokea kitabu
chake cha uanachama toka kwa Makamu Mwenyekiti wa Ikulu
SACCOS, Bw. Deodatus Gaudio (wa tatu toka kulia). Wengine ni
Katibu wa wa ushirika huo Bw. Benedicto Damiano (wa pili
kulia), Mtunza Hazina Bi. Judith Medson ( wapili kushoto)
na Mshauri Mkuu na Mlezi wa Ikulu SACCOS Bw Joseph Sanga
kulia,wakati wa hafla fupi ya kumkabidhi kitabu chake cha
uanachama wa ushirika huo Ikulu Dar es salaam.

Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue akionesha kitabu
chake cha uanachama baadas ya kukabidhiwa na Makamu
Mwenyekiti wa Ikulu SACCOS, Bw. Deodatus Gaudio
wakishuhudiwa na Katibu wa wa ushirika huo Bw. Benedicto
Damiano, Mtunza Hazina Bi. Judith Medson ( wapili kushoto) Mshauri Mkuu na Mlezi wa Ikulu SACCOS Bw Joseph Sanga
kulia,wakati wa hafla fupi ya kumkabidhi kitabu chake cha
uanachama wa ushirika huo Ikulu Dar es salaam.
chake cha uanachama baadas ya kukabidhiwa na Makamu
Mwenyekiti wa Ikulu SACCOS, Bw. Deodatus Gaudio
wakishuhudiwa na Katibu wa wa ushirika huo Bw. Benedicto
Damiano, Mtunza Hazina Bi. Judith Medson ( wapili kushoto) Mshauri Mkuu na Mlezi wa Ikulu SACCOS Bw Joseph Sanga
kulia,wakati wa hafla fupi ya kumkabidhi kitabu chake cha
uanachama wa ushirika huo Ikulu Dar es salaam.
Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue amefurahishwa na uwepo wa vyama vya Ushirika vya Akiba na
mikopo (SACCOS) katika taasisi na idara za serikali, akisema kuwa hilo ni jambo
la maana kwa kuwa inatoa fursa kwa
watumishi kuwa na kipato cha ziada kitachosaidia kuwaletea ahueni kwani mishahara pekee haikidhi matakwa yao yote.
Amesema SACCOS ni
kama
benki ya mtu mnyonge, na kusisitiza kwamba
mifuko ya aina hiyo inaposimamiwa vizuri faida yake kwa wanachama ni kubwa sana
kwani humpa mtumishi ahueni na kumfanya afanye kazi kwa moyo na bila wasiwasi ama usongo wa mawazo.
Balozi Sefue ameyasema hayo Jumanne Machi 3, 2015 jioni
alipokuwa akiongea na uongozi wa Ikulu SACCOS,
uli
omtembelea ofisini kwake
Ikulu Dar es salaam kumkabidhi rasmi kitabu chake cha uanachama kufuatia
kujiunga kwake na ushirika huo.
“Mishahara yetu ndani
ya utumishi wa umma haitoshi kukidhi mahitaji yetu yote, kwa hiyo mipango yote
hii ya SACCOS, Mfuko wa Rambirambi na Mfuko wa Ushirika
iliyopo hapa Ikulu
inafanya maisha ya
mtumishi yawe na ahueni sana na kumfanya afanye kazi kwa moyo.
“Hayo ni mambo ambayo nayaamini sana na nayaunga mkono; na naamini hata Mhe Rais mwenyewe anayaunga
mkono na ndio maana amekuwa mwepesi kujiunga na ushirika ”, amesema Balozi
Sefue baada ya kukabidhiwa kitabu namba 2 na Makamu Mwenyekiti wa Ikulu SACCOS,
Bw. Deodatus Gaudio. Kitabu namba moja amekabidhiwa Rais Jakaya Mrisho Kikwete.
Awali, mshauri Mkuu na Mlezi wa Ushirika huo wa Ikulu, Bw.
Joseph Sanga, alimfahamisha Katibu Mkuu Kiongozi kwamba mifuko ya SACCOS, Ushirika wa Nyumba na Rambirambi ya
watumishi wa Ikulu iko imara na inaendelea kunufaisha wanachama wake kwa
ufanisi.
Bw. Sanga amesema malengo makuu ya mifuko hiyo ni kuleta
ustawi kwa watumishi na kwamba wote wanaelewa kuwa mikopo ya SACCOS yao sio kwa
ajili ya kununulia chakula ama mavazi bali ni ya kuwekeza kwenye miradi
itayowaongezea kipato.
“TUnataka kwenda mbali zaidi kwa kushirikiana na mfuko wetu
ya Ushirika wa Nyumba ambo tayari umepeleka maombi ya ardhi kwa wanachama wake
ambapo viwanja vikipatikana tuna mategemeo ya kuwapa mikopo kuvununua. Mpango
huu una faida kwani ni wa amana kubwa na riba ndogo”, alisema Bw. Sanga
alipokuwa anafafanua kuhusu mipango ya Ikulu SACCOS.
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia