NINI MAANA YA DHANA YA NDOA?
Kwa mujibu wa sheria ya Ndoa ya
Tanzania sura ya 29 kifungu cha 160 kifungu kidogo cha 1 kama
ilivyofanyiwa marejeo mwaka 2002, ikidhibitika kuwa mwanaume na mwanamke
wameiishi pamoja kwa miaka miwli au zaidi, katika hadhi ya mume na mke,
basi kutakuwepo na dhana ya ndoa.
Sheria hii, imedhamiria kukomesha kama si kupunguza ile tabia ya wanaume au wanawake wengi kukaa na kumtumia mwenzi wake kwa jinsi ya mume au mke na baadae kumtelekeza akiwa hana kitu chochote katika maisha yake .
Hata ivyo ili mtu aishawishi mahakama kuhusu dhana ya ndoa inabidi athibitishe vitu vifuatavyo:
1. Ziwe ni jinsia mbili tofauti yaani jinsia ya kiume na ya kike.Hii ni
kufuatia msimamo wa Tanzania kutotambua ndoa za jinsia moja.
2.
Wawe wameeishi chini ya nyumba moja. Hapa ni papana kidogo. Hapa
inahitaji kuthibitika kuwa watu hawa huwa wanaishi ktk nyumba moja
ikiwemo tendo la ndoa. Hivyo ile tabia ya kuwa unatembelewa tu weekend
na mnaspend na lover wako siku mbili tatu halafu kila mtu anarudi kwake
hapa haiwezi kutumika kuthibitisha dhana ya ndoa.
3. Wawe
wameishi katika hadhi ya mume na mke. Hapa ni lazima pathibitike kuwa
wawili hao wameishi katika hali ya kuwapa hadhi ya mke na mume. Mfano,
kusaini mkataba fulani kama mume na mke (spouses), kuzaa pamoja.
4. Lazima wawe wameishi hivyo kwa muda wa miaka 2 na zaidi. Hapa sheria
iko wazi kabisa kama itakuwa chini ya miaka 2 basi hutapata haki za
kisheria za mke kwa kuwa hapatakuwa na dhana ya ndoa.
JE MTU ANAWEZAJE KUIBATILISHA NDOA YA NAMNA HII?
Ili kuibatilisha ndoa ya namna hii mtu anatakiwa hathibitishe kutokamilika kwa vipengele tajwa hapo juu. Mfano kama miaka walioshi ni chini ya 2.
Ili kuibatilisha ndoa ya namna hii mtu anatakiwa hathibitishe kutokamilika kwa vipengele tajwa hapo juu. Mfano kama miaka walioshi ni chini ya 2.
JE NI HAKI GANI WANAZOKUWA NAZO WANANDOA WA NAMNA HII?
Haki za wanandoa wa namna hii ni kama za wanandoa wa ndoa za namna nyingine zote. Mfano, haki ya unyumba,
Sasa najua kwa Tanzania wengi sana mmeoa na kuolewa bila kujijua ila ukweli ndio huo.
Kwa leo naishia hapo. Nitaendelea tena na aina nyingine za ndoa wakati ujao.