Hivi ndivyo Basi la Majanja linavyo onekana mara baada ya kuondoa Lori lilikuwa limekandamiza basi hilo.
Umati wa watu mbalimbali wakiwemo wasafiri wasafiri waliokuwa katika mabasi mengine wakiwa wamejaa kushuhudia Ajali hiyo.
Shughuli za uokoaji zikiwa zinaendelea
Muonekano wa Basi la Abiria na Lori yaliyo athirika kwa ajali hiyo
Mashuhuda
Basi la Abiria likiwa katika Hali mbaya baada ya ajali
Waokoaji wakiwa wanaendelea kufanya ushirikiano namna ya kuwasaidia watu waliopata ajali hiyo.
Miongoni mwa watu wakiwa wanatazama namna Magari hayo yalivyopata ajali
Askari
wa usalama Barabarani wakiwa wanahakikisha watu mbalimbali waliodhurika
katika ajali hiyo wanaweza kupata msaada/huduma kwa haraka.
Basi
lililokuwa limebeba abiria waliokuwa wakitokea Mbeya kuelekea Dar es
salaam Lenye namba za usajili T438 CDE likiwa katika hali mbaya.
Taarifa za awali kutoka jeshi la polisi mkoani Iringa zinaeleza kuwa basi la kampuni Majinja lenye usajili wa namba T438 CDE
lililolaliwa na Lori lilikuwa limebeba jumla ya watu 49, idadi hiyo ni
pamoja na dereva na kondakta wa basi hilo.wengi wa watu hao wamefariki
dunia idadi ya majeruhi haijajulikana bado. Taarifa hizo zinaeleza kuwa kwenye mizigo mingi ya abiria waliokuwa kwenye basi hilo kumepatikana madaftari mengi ya wanafunzi wa chuo kikuu cha Dar es salaam hivyo jeshi hilo linaendelea kufanya mawasoliano ma wamiliki wa gari hilo ili kujua kama lilikuwa limekodishwa kubeba wanafunzi wa chuo hicho ama ni mchanganyiko wa kawaida wa abiria.
Chanzo :Iringa yetu Blog
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia