BARAZA LA UTAWALA POSTA AFRIKA WAKUTANA ARUSHA KUJADILI CHANGAMOTO



Baraza la utawala la umoja wa Posta Afrika  limekutana  (leo) jana
jijini hapa kujadili changamoto ambazo zinakabili mashiriki ya posta
katika nchi husika.

Akiongea na waandishi wa habari katibu mkuu wa  wizara ya mawasiliano
sayansi na teknologia  Florence Turuka alisema kuwa umoja huo wa nchi
za afrika umekutana jijini hapa kujadili changamoto mbali mbali ambazo
zinaikabili mashirika ya posta.

Alisema kuwa katika mkutano huo ambao alibainisha unafanyika kwa muda
wa siku tisa  ambapo kabla ya mkutano mkuu umetanguliwa na kamati
mbalimbali  ambazo zitajadili changamoto ambazo zinakabili mashirika
haya ya posta.

 Alibainisha kuwa mara baada ya kamati kukaa kutakuwa na mkutano wa
mawaziri wa nchi za afrika ambapo utafanyika kwa muda wa siku mbili
kwa ajili ya kujadili changamoto ambazo zinaikabili mashirika haya ya
posta katika nchi zao.

Alitaja mambo ambayo baraza la utawala la umoja wa posta afrika
watajadili kwa kipindi hichi kabla ya mkutano wa mawaziri kuanza kuwa
ni pamoja na kupitia mwenendo wa bajeti katika mashirika haya ya
posta,kuangalia shughuli za maendeleo ya posta ,kupitia maswala
yanayohusiana na posta ,kuangalia sehemu ambayo huduma ya kieletroniki
inavyofanya kazi  pamoja na kuangalia mikakati gani posta inaweza
kusaidia katika maendeleo ya wananchi katika swala zima la posta.

Aidha Turuka alitaja changamoto ambazo shirika hilo la posta
linazipata kuwa ni pamoja na kuwepo kwa maendeleo ya teknologia ya
kieletroniki ambapo alitolea mfano kuwa kwa sasa swala la usafirishaji
wa barua umepungua tofauti na awali lakini pamoja na hivyo mashirika
ya posata yamekuwa yakisafirisha vivurushi

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

Previous Post Next Post