Waziri wa Nyumba wa utawala wa Kizayuni wa Israel amesema kuwa,
watajenga hekalu kwa ajili ya Mayahudi ndani ya ua wa msikiti Mtukufu wa
al Aqswa. Uri Ariel ambaye ni mwanachama wa chama chenye misimamo
mikali cha 'Jewish Home' amesema kwamba, Baraza la Mawaziri la Israel
limesimamisha ujenzi wa vitongoji vipya vya walowezi wa Kizayuni katika
Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan lakini kwamba atahakikisha kuwa hekalu
la Mayahudi linajengwa ndani ya Masjidul Aqswa.
Huku akitoa matamshi ya kufurutu ada na ya kibaguzi waziri huyo wa
Israel sambamba na kubainisha kuwa, kuna matakwa ya kuundwa serikali
mbili za Palestina na Israel amesema kwamba, njia pekee na ya uhakika
eti ni kuwepo serikali moja tu ya Israel katika eneo hilo.
Inafaa kukumbusha hapa kuwa, viongozi wa utawala ghasibu wa Israel
wanafanya kila njama ili waweze kuharibu athari na utambulisho wa
Kiislamu na Kiarabu katika mji wa Quds kwa lengo la kuuyahudisha mji huo
Tags
Habari