KATIBU
mkuu wa CUF na makam wa kwanza wa raisi wa serekali ya mapinduzi ya
Zanzibar Maalimu Seif Sharif Hamad akimuombea kura mgombea wa udiwani wa
kata ya Elerai John Gilbert Bayo kwa wakazi wa kata hiyo kwenye viwanja
vya shule ya msingi Elerai na kuwataka kumchagua mgombea
Wakazi wa
kata ya Elerai wametakiwa kuhubiri amani na mshikamano na kukataa wale wote ambao hawaitakii amani Mkoa wa
Arusha kwani wamekuwa wakiwaumiza kiuchumi na kimaendeleo na kuwa vurugu na
maandamano kwao hayana tija badala yake ni hasara kwa uchumi na maendeleo ya
mkoa wao.
Kauli hiyo
imetolewa na makamu wa kwanza wa serekali ya umoja wa kitaifa(SMZ)Maalim Seif Sharif
Hamad wakati akiongea na wakazi wa kata hiyo alipokuwa mgeni rasmi kwenye
kampeni za uchaguzi wa kata hiyo.
Sharif hamad
aliwataka watanzania kutobaguana kwa visingizio vya ukabila udini na aina
yeyote ya ubaguzi kwa minajili ya kuvurga amani na mshikamano wa taifa letu na
kuwa siasa ni maisha ya watanzania wote hivyo kila mmoja wetu anawajibu wa
kutunza amani na mshikamano sanjari na kuacha ushabiki kwenye siasa.
“Ndugu zangu
wana Arusha siasa ndiyo maisha yetu na vijana ndio msingi wa taifa kwani ndiyo
nguvu kazi sasa hawa wakitumika vibaya kwa maslahi ya wachache kufanya vurugu
na maandamano tutakuwa tunaelekea wapi”alihoji Maalim Seif.
Makamu huyo
alisema watanzania wote bila kujali rangi,ukabila,na udini wanahaki sawa za
kupata mgawanyo wa kiuchumi hapa hakuna ambaye hana hati miliki na nchi hii
kwani nchi hii ni yetu sote bila kujali itikadi za vyama.
Alisema
anashangaa kuona nchi hii yenye rasilimali lukuki na ardhi isiyokataa mazao
yeyote hapa dunia ikiwa katika hali mbaya ya kukosa chakula wakati imejaaliwa
neema kubwa hii ndiyo sera za chama cha mapinduzi kilipotufikisha na kuwataka watanzania kuacha ushabiki wa kisiasa
na kujiuliza tumekosea wapi ilituweze kuyapatia majibu sahihi jmatatizo yetu.