Maafisa wa usalama mjini Cairo, Misri leo wamewaua kiasi ya
waandamanaji watatu baada ya mamia ya waandamanaji hao
waliojitokeza kumuunga mkono Rais aliyeng'olewa madarakani
Mohammed Mursi kuanza kuelekea katika kambi ya kijeshi mjini humo
ambako kiongozi huyo anazuiliwa na wanajeshi waliompindua.Maelfu
ya wafuasi wa Mursi wameandamana katika miji kadhaa nchini humo
kwa kile udugu wa kiislamu umekiita 'Ijumaa ya ghadahabu' kutokana
na mapinduzi ya kiongozi wa kwanza aliyechaguliwa kidemokrasia
mwaka mmoja uliopita.Mtu aliyeshuhudia ameliambia shirika la habari
la Reuters aliwaona watu kadhaa wakiwa na majeraha ya
risasi.Maelfu ya watu pia waliandamana mijini Alexandria na Assiut
kupinga serikali ya muda iliyoapishwa jana.Mjini Ismailia wanajeshi
walifyatua risasi hewani wakati wafuasi wa Mursi walipojaribu
kuingia katika ofisi ya gavana wa jimbo hilo.