Raisi Jakaya Kikwete amesema kuwa hali ya barabara
zilizo chini ya serikali za mitaa ni nzuri ikilinganishwa na miaka 10 iliyopita
hatua iliyopigwa,pamoja na mambo mengine imetokana na maamuzi ya kisera ya
kufungua fursa za kiuchumi vijijini na wilayani.
Pia kutenga fedha zaidi kwa ujenzi wa ukarabati wa
barabara na kuimarisha usimamizi wa miradi ya barabara kwa kuongeza fedha za
matengenezo ya barabara mara 10 kutoka billion 23.8 mwaka 2005/6 hadi bilion257.7
sawa na ongezeko la asilimia 980%.
Hayo aliyasema wakati akifungua mkutano wan ne wa
wadau wa mfuko wa barabara uliowashirikisha watungasera na watoa maamuzi kutoka
katika mikoa wilaya na halmashauri zote hapa nchini unaoendelea jijini hapa
huku mtandao wa bara bara za lami katika halmashauri ukiwa umeongezeka kutoka
km790 kutoka mwaka2005/6 hadi km1326 hivi sasa.
Dkta Kikwete alisema kuwa barabara za changarawe
zimezidi kuongezeka kutoka km13,000 mwaka2005/6 hadi km22089 hivi sasa huku
wahandisi waliosajiliwa kwenye sekta ya barabara katika halmashauri hivi sasa
wakiwa ni 137 ukilinganisha na 70 walikuwa mwaka 2010.
‘’Nimeridhika na usimamizi na ilikuimarisha usimamizi
na ufuatiliaji wa kazi za barabara kwenye ngazi ya ofisi ya wizara ya TAMISEMI
nimeridhia kukipandisha kitengo cha miundombinu kuwa idara kamili yenye sehemu
tatu ambazo ni miundombinu mijini,miundombinu vijijini,na pamoja na utafiti’’alisema
Raisi Kikwete.
Alisema kuwa halmashauri nyingi hivi sasa zimekuwa na
uwezo wa kusanifi na kusimamia ujenzi na miradi mikubwa ya madaraja huku
halmashauri nyingi zikipiga hatua nzuri katika usimamizi wa matumizi ya fedha
za mfuko wa barabara ikiwemo baadhi kupiga hatua na kuongeza uwezo wa kutumia
fedha za mfuko wa barabara na usimamizi wa ubora wa kazi za barabara.
Aidha akimkaribisha Rais kuzungumza waziri wa ofisi ya
waziri mkuu tawala za mikoa na serikali za mitaa Hawa Ghasia alisema kuwa
ujenzi wa barabara ndani ya serikali za mitaa ni moja ya minayogusa shughuli za
maendeleo ya wananchi walio wengi ndio maana kauli mbiu ya mkutano huu ni ubora
wa kazi ili kuwa na barabara endelevu.
Alisema kuwa shughuli zote za utekelezawa miradi ya
maendeleo zinafanyika kwa wakati kwa ubaora unaostahili na kwakuzingatia sheria
kanuni na utaratibu zinazotawala matumizi ya fedha za serikali.