BREAKING NEWS

Tuesday, August 11, 2015

HIIVI NDIVYO JINSI MWENYEKITI WA CCM MKOA WA ARUSHA ONESMO NANGOLE NA KATIBU MWENEZI WA CHAMA HICHO ISAAC JOSEPH( KADOGOOO) ALIVYO KIAMA CHAMA CHA MAPINDUZI NA KUAMIA CHADEMA

kadogooo11111
Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Arusha Onesmo  Ole Nangole kulia akizungumza na waandishi wa habari leo mara baada ya kuhamia rasmi chama cha demokrasia na maendeleo (CHADEMA)kushoto ni Katibu Mwenezi wa CCM mkoa wa Arusha Isaac Joseph Maarufu kama Kadogoo

Katika hali isiyokuwa ya kawaida Chama cha Mapinduzi kimeendelea kupoteza  wanachama  wake mara baada  Mwenyekiti wa chama hicho Mkoa wa Arusha, Onesmo Nangole pamoja na Katibu Mwenezi wa Mkoa huo Isaac Joseph kutangaza rasmi kukihama chama hicho cha CCM na kujiunga na CHADEMA.

Uamuzi huo ulifanyika jana jijini Arusha katika moja ya hotel maarufu ambapo viongozi hao walipata wasaa wa kupokelewa na uongozi wa chama cha demokrasia na maendeleo (CHADEMA)

Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Arusha Onesmo  Ole Nangole  wakati akizungumza na waandishi wa habari pamoja na wananchama wa chadema alisema kuwa CCM hivi sasa imekosa misingi iliyounda chama hicho ya haki na usawa na kuongeza kuwa hivi sasa kimekuwa ni chama cha watu wachache ambao wamekuwa wakichukuaa maamuzi kwa faida yao.

“Nasema CCM imekosa misingi iliyounda chama hiki hakuna haki yeyote inayotendeka imekuwa chama cha watu Fulani ambao wamekuwa wakichukua maamuzi ya kukurupuka kwa faida yao”alisema Nangole

Kwa upande wake  Katibu Mwenezi wa CCM mkoa wa Arusha Isaac Joseph Maarufu kama Kadogoo alisema  kuwa kudhirisha kuwa CCM sasa inaendeshwa kwa maslahi ya watu wachache, mchakato wa kumpata mgombea Urais wa CCM uligubikwa na mizengwe na kusema kuwa kama kanuni na taribu zingefuatwa ni Edward Lowasa ndiye angechaguliwa katika mchakato ule.

Pia alisema kuwa hawezi kukaa na kuongoza katika chama ambacho wafuasi wake wamekihama ,huku akidai kuwa kwa Arusha mjini alikuwa na wafuasi elfu ishirini na saba na waliojitokeza kupiga kura ya maoni ya kumpendekeza mgombea ubunge kupitia CCM ni elfu tano

“ Siwezi kubaki kuongoza katika chama  ambacho kinabaka demokrasia Uongozi wa CCM watafute viongozi wengine wa kuongoza chama hicho siko tayari na siwezi tena”alisema Kadogoo

Mwenyekit wa CHADEMA Wilaya ya Arusha Magoma Derick Magoma akiwapokea wanachama hao kutoka CCM na kuhamia rasmi CHADEMA anawakaribisha wote wanaoijisika kuunga nao na kuleta mabadiliko ya kweli kwa maslahi ya Taifa kwa ujumla
“Tunawakaribisha wote wanaotaka kuhamia chadema mlango upo wazi mda wowote na siku yeyote mda wa mabadiliko ni sasa”alisema Magoma

Share this:

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

 
Back To Top
Copyright © 2014 MOUNT KILI NEWS. Designed by OddThemes | Distributed By Gooyaabi Templates