Mkuu wa wa Kitengo cha Huduma za
Kifedha wa Tigo, Ruan Swanepoel (kushoto), akizungumza katika mkutano na
waandishi wa habari Dar es Salaam leo asubuhi katika uzinduzi wa kampeni ya
Chagua Tigo Pesa, Inalipa. Kulia ni Meneja Chapa wa Tigo,
William Mpinga.
Meneja
Chapa wa Tigo, William Mpinga (kulia), akizungumza katika uzinduzi
huo. Kushoto ni Mkuu wa wa Kitengo cha Huduma za Kifedha wa Tigo, Ruan
Swanepoel.
Wanahabari wakichukua taarifa
hiyo.
Na Dotto Mwaibale
KAMPUNI ya simu ya mkononi ya tigo Tanzania
imezindua Kampeni iitwayo"chagua tigo pesa,inalipa"ikiwa na lengo na la
kuongeza upatikanaji wa fedha kwa njia ya simu ya mkononi kwa
wateja.
Akizungumza Dar es Salaam leo asubuhi Mkuu
wa Kitengo cha Huduma za Kifedha wa Tigo Ruan Swanepoel alisema huduma hiyo
ikiwa na muonekano mpya na sura kwa wateja wake wanaotumia huduma ya tigo
pesa Tanzania nzima.
Alisema kuwa kwasasa mtandao wa tigo
umeenea kwa wingi hapa nchini na unatumiwa na asilimia 90 ya wananchi wote
wanaomiliki simu za mkononi.
Alisema kuwa mtandao wa tigo unakikisha
inatoa huduma stahiki kwa wateja wakena kuhakikisha huduma ya tigo pesa
inazidi kuwa na huduma pendwa kwa sababuinapatikana kirahisi na
makini.
Alisema kuwa huduma hii inalipa kwa wateja
wake na kukopa fedha hasa kwa wale wenye kipato kidogo na wasio na huduma
za kibenki.
Alifafanua kuwa wateja wa tigo pesa
watanufaika na kampeni hii kwa kuypata vifurushi vya bure kila wannunuapo
bidhaa na kulipia kwa tigo pesa kutoka kwa wauzaji
waliosajiliwa.
Pia aliongeza na kusema kuwa wateja
watapata riba kila baada ya miezi mitatu kulingana na kiasi cha fedha ya
kifurushi ambacho mteja atamnunulia mtu mwingine kwa tigo pesa.