Hapa ilikuwa
ni mapema kabisa ambapo washiriki wa Shindano la Mama Shujaa wa
Chakula msimu wa Nne wakiwa wanajikusanya kwa ajili ya kupewa mwongozo
wa siku nzima
Baada ya
washiriki wa Shindano la Mama shujaa wa Chakula Shindano linalo
endeshwa na Oxfam kupitia kampeni yake ya Grow na kudhaminiwa na Gates
and Melinda Foundation,TBS, Cooperative Bank Great Britain na Care
Tanzania, baada ya kuwasili wote sasa wanapangwa makundi makundi
kwa ajili ya kuanza mchakato wa siku
Hapa katika
kundi la kwanza washiriki wa Shindano la Mama Shujaa wa Chakula
, Shindano linaloendeshwa na Oxfam kupitia kampeni yake ya Grow hapa
wakiwahamasisha wanakijiji cha kisanga kilimo cha Biashara na
kubadilishana mawazo kuhusu nyenzo , mazao na tathimini ya mapato na
matumizi.
Kundi la
pili wakiendelea kutoa Elimu ya Kilimo kwa Wanakijiji
Kundi la
tatu wakiendelea kutoa elimu na kubadilishana mawazo na wanakijiji wa
kijiji cha Kisanga
Mmoja wa
Washiriki wa Shindano la Mama Shujaa wa Chakula , Regina
kalipi(Katavi) akiwa ameshikiriwa na washiriki wenzake baada ya
kuanguka akisoma Lisara iliyokuwa inahusu kilimo
Katikati ni Winnie
Malya Mshiriki kutoka Kilimanjaro akisoma Lisara kwa wanakijiji ambao
hawapo Pichani juu ya kilimo.
Burudani
lilianzia hapa ambapo Washiriki wa Shindano la Mama Shujaa wa Chakula
Pili Kashinje(zanzibar, Neema Hilonga (Manyara) na Mandutha kitoeloh
9Singida) walishiundana vilivyo katika kukimbia lakini Pili
aliibuka kuwa Mshindi.
Burudani
ilizidi kuwa Taaamu zaidi ambapa Washiriki wa shindano la
Mama Shujaa wa Chakula Shindano linaloendeshwa na Oxfam kupitia
kampeni yake ya Grow na kurushwa katika Runinga yako kupitia Chanel ya
ITV kuanzia saa 12:30 Jioni na Kurudiwa saa 11:30 asubuhi , hapa ni
pata ni kupate ambapo Winnie Mallya(Kilimanjaro) Edna Kiogwe (Dar es
salaam) na Severina Mutahyabarwa (Kagera) walishindana vikali
kukukimbia wakiwa wamevaa magunia haa hivyo mshiriki kutoka
Kilimanjaro aliwatoa nje na kuibuka mshindi.
Mambo
yalizidi noga zaidi ambapo washiriki waliendelea kutoa Burudaani ya
nguvu kwa wanakijiji wa Kijiji cha Kisanga ambapo hapa sasa
Caroline Chilele(Morogoro) , Eva Daudi (Pwani) na Dina Sumari (Meru)
walichuna vikari wakiwa wanatembea kwa mwendo wa kasi huku wakiwa na
vijiko nyenye ndimu Mdomoni..Hata hivyo mshindi ilikuwa ni
lazima apatikane na Calorine alifanikiwa kuibuka
kidedea
Ulizani
washiriki wa shindano la Mama Shujaa wa Chakula hawawezi kuziburuta
Njinga.... Ilikuwa ni Burudani zaidi hapa ambapo sasa Hawa
Mkata(Mtwara) ,Edna Kiogwe (Dar es salaam), na Upendo Mhomisoli
(Njombe) walishindana vikali kuendesha Baiskeri. Hata hivyo
Mshiriki toka Mtwara aliibuka Mshindi
Siku hii kwa
hakika wanakijiji walishuhudia Burudani ya kipekee na ya aina yake
kabisa, hapa wakina mama hawa walikuwa wanajikumbusha enzi za utoto
wao ambapo walicheza ule mchezo Maarufu sana uitwao Reje hapa
walidunguana, walitoa kijasho maana shughuli ya kukwepa Mpira si ya
masihala, Calorine Chilele(Morogoro) aliibuka
Mshindi.
Na Mwisho
Washiriki wa Shindano la Mama Shujaa wa Chakula Shindano
linaloendeshwa na Oxfam kupitia kampeni yake ya Grow na
kurushwa katika Runinga yako kupitia Chanel ya ITV kuanzia saa 12:30
Jioni na Kurudiwa saa 11:30 asubuhi ambapo hapa ilikuwa ni vuta
ni kuvute mpaka kieleweke hapa washiriki wote walikuwa wanashindana
kwa kasi ya ajabu sasa kilichotokea hapa ni cha kushangaza kamba
ilikatika hivyo kukawa hakuna mshidi wakatoka sale
sale..
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia