Ticker

6/recent/ticker-posts

NMB YAKABIDHI MSAADA WA MADAWATI HAI

Meneja wa benki ya NMB tawi la Hai Medadi Malisa kulia akimkabidhi mwalimu
mkuu wa shule hiyo Teodora Mlayi huku akishuhudiwa na mgeni rasmi Zuhura
Chikira ambaye ni katibu tawala wa wilaya ya Hai

Meneja wa Benki ya NMB wilaya ya hai Medadi malisa Kushoto akiwa amekaa
kwenye madawati yaliyotolewa msaada na benki hiyo kwa shule ya msingi kambi
ya Raha, kulia kwake ni Afisa Elimu wa wilaya hiyo Deogracia Mapunda
akifuatiwa na katibu tawala Zuhura Chikira na mwenyekiti wa shule hiyo.

 Na Woinde Shizza,Hai

BENKI ya NMB kanda ya Kaskazini  imetoa msaada wa madawati 50 wenye thamani
ya sh. milioni 5 katika shule za msingi Kambi ya Raha,iliyomo wilayani
humo,huku msaada huo ukitokana na faida inayopata benki hiyo.


Akiongea jana baada ya kukabidhi msaada huo,meneja wa benki  hiyo tawi la
Hai mkoa Kilimanjaro, Medadi Malisa alisema benki hiyo imeamua kutoa msaada
huo kulingana na uhitaji wa shule hiyo baada ya kupokea maombi kutoka kwa
viongozi wa shule hiyo.


Alisema Benki ya NMB imekuwa ikipokea maombi mengi ya uhitaji wa msaada kwa
jamii lakini kwa kuzingatia na umuhimu wa eneo husika ndio maana imefikia
uwamuzi wa kutoa madwati katika shule hiyo baada ya kutambua kuwa kuna haja
ya kusaidia wanafunzi hao.



‘’ Benki ya NMB imeamua kutoa msaada wa madawati 50  kutokana na uhitaji wa
shule husika napenda niwahakikishie kuwa benki yenu imetenga zaidi ya
shilingi bilioni 1 kwa ajili ya kuchangia maendeleo ya wananchi ikiwemo
kusaidia sekta ya Afya, Elimu na michezo,’’alisema Malisa.


Aliongeza kuwa kuwa,benki hiyo iliamua kutoa msaada wa madawati hayo ya
wanafunzi ili kuweza kutoa motisha kwa wanafunzi hao kuweza kusoma kwa
bidii kwa madai kuwa kutokuwepo kwa vitendea kazi mashuleni ni moja ya
sababu zinazopelekea wanafunzi wengi kufeli.



"Msaada huu wa madawati  umetokana na faida kidogo ambazo benki inapata
hivyo tumeona katika faida hizo ni jambo jema kutoa msaada wa aina hii kwa
ajili ya kuweza kuendeleza watoto kielimu kwani wao ndiyo Taifa la kesho,"
alisema Malisa.



Kwa upande wa Katibu tawala wa Wilaya ya Hai Zuhura Chikira, ambaye
alimwakilkisha mkuu wa wilaya ya Hai   aliipongeza benki ya NMB kwa kutoa
msaada huo na kuwataka wadau wengine wa elimu kuiga mfano wa benki hiyo kwa
kutoa mchango kama huo ili kupunguza ya madawati wilayani huo.


Alisema wilaya ya Hai inakabiiwa na changamoto mbalimbali ikiwemo ya
upungufu wa madawati hata hivyo alisema taitizo hilo lipo kwa baadhi ya
shule za msingi na wilaya ipo kwenye mkakati wa kukabiliana nalo.


Aliwataka wadau wengine wa elimu kuiga mfano wa benki ya NMB,kwa kuisaidia
serikali kupunguza changamoto zilizopo kwenye shule mbalimbali hapa nchini
hasa za msingi ambako ndiko tatizo kubwa lilipo.

Post a Comment

0 Comments