TASWA DAR HOI TAMASHA LA WAANDISHI ARUSHA



 kikosi cha timu ya mchezo wa mpira wa pete ya Taswa dar mara baada ya mechi kuisha



Siku moja kabla ya bonanza waandishi wa habari wa mkoa wa Arusha walipata fursa ya kutembelea kiwanda cha bia ya TBL Arusha hapa mmoja wa wafanyakazi wa kampuni hiyo akiwa anawapa maelekezo ya jinsi kiwanda hicho kinavyoweza kufanya kazi  ya kutengeneza beer kwa kutumia mashine na komputa
 nikiwa na waandishi wa habari wakogwe mara baada tu ya kuwasili ndani ya kiwanda cha bia cha Tbl Arushawa kwanza kushoto ni Gwandu  akifuatiwa na Woinde shizza,Mr mchau wakwanza kulia ni Salma Mchovu pamoja na Yasinta



 waandishi wahabari wa mkoa wa Arusha wakifurahia wakati tamasha likiendelea


 Na Woinde shizza,Arusha

Timu ya soka ya chuo cha uandishi wa habari   Arusha(AJTC) juzi walitwaa ubingwa katika bonanza la 10 vyombo vya habari mkoani Arusha huku Timu ya wanahabahari wa Dar es Salaam TASWA FC wakishindwa kutamba.

Katika Bonanza hilo, ambalo lilishirikisha jumla ya timu nane, TASWA FC) alishindwa kutamba na kushika nafasi ya nne, Hata hivyo timu ya wanahabari wasichana kutoka Dar es Salaam(TASWA Qeen) iliweza kutwaa ubingwa wa mpira wa pete.
Katika bonanza hilo, lililofanyika Uwanja wa Sheikh Amri Abeid mgeni rasmi alikuwa Mkuu wa mkoa wa Arusha, Felix Ntibenda  ,AJTC walitwaa ubingwa baada ya kujikusanyia alama saba huku nafasi ya pili, ikichukuliwa na timu ya wanahabari kutoka mkoa wa Manyara wa kituo cha radio ORS.
Chuo cha habari cha IMS kilishika nafasi ya tatu ,kikifuatiwa na TASWA Dar, TASWA Arusha, MJ Radio,Arusha One radio na radio  Habari Maalum.
Mkuu wa mkoa wa Arusha, Filex Ntibenda aliwakabidhi mabingwa wa soka kikombe na fedha taslim Tsh 250,000, huku washindi wa pili wakipata fedha taslimu 150,000 na kikombe.
Katika Tamasha hilo, timu ya TASWA Qeen ilikabidhiwa kikombe na Tsh 150,000, huku timu ya pili AJTC Qeen ikipata fedha taslim 10000 na kikombe.
TASWA FC ilipata zawadi ya timu yenye nidhamu katika michuano hiyo na kupokea zawadi na fedha taslimu 50,000.
Akizungumza wakati akifunga bonanza hilo, Ntibenda alipongeza TASWA Arusha na kampuni ya Arusha media kwa kuandaa Bonanza hilo.
Aliwataka wanahabari kuwa na tabia ya kushiriki katika michezo kwani michezo hujenga, Afya na ni ajira.
Mkuu wa mkoa wa Arusha, pia alikabidhi vyeti vya udhani Bonanza hilo  , kampuni ya bia nchini(TBL), Shirika la hifadhi ya Taifa TANAPA, kampuni ya Mega Trade.
Shirika la nyumba la Taifa(NHC),Kampuni ya Tanzanite One, Big Expedition, Taasisi ya Faidika, Kampuni ya Pepsi na Coca cola.

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

Previous Post Next Post