Mkurugenzi
wa Taasisi ya Kupunguza Matatizo ya Mapafu Duniani iliyopo nchini
Tanzania (WLF), Dk. Nguke Mwakatundu akifungua semina hiyo leo jijini
Dar es Salaam.Mkurugenzi
wa Huduma za Kliniki wa Taasisi ya Kupunguza Matatizo ya Mapafu Duniani
iliyopo nchini Tanzania (WLF), Dk. Sunday Dominico akiwasilisha mada
katika semina hiyo leo ofisi za WLF.Meneja Mawasiliano wa Taasisi ya Kupunguza Matatizo ya Mapafu Duniani iliyopo nchini Tanzania (WLF), Victoria Marijani.
Mkurugenzi
wa Taasisi ya Kupunguza Matatizo ya Mapafu Duniani iliyopo nchini
Tanzania (WLF), Dk. Nguke Mwakatundu akifungua semina hiyo leo jijini
Dar es Salaam.Meneja Mawasiliano wa Taasisi ya Kupunguza Matatizo ya Mapafu Duniani iliyopo nchini Tanzania (WLF), Victoria Marijani.
BAADHI ya
wanahabari wa mitandao ya jamii jijini Dar es Salaam wamepewa mafunzo
juu ya taarifa za uzazi na afya ya mama na mtoto ili waweze kuelimisha
zaidi jamii kupitia mitandao yao dhidi ya taarifa hizo. Akizungumza
wakati akifungua semina hiyo, Mkurugenzi wa Taasisi ya Kupunguza
Matatizo ya Mapafu Duniani iliyopo nchini Tanzania (WLF), Dk. Nguke
Mwakatundu alisema taasisi yake imeamua kutoa mafunzo hayo kwa
wanahabari hao ili waweze kuwa mabalozi wazuri wa kuelimisha jamii
kupitia mitandao yao juu ya umuhimu wa kupambana na vifo vya mama na
mtoto vinavyoendelea kutokea kila uchao. Alisema kazi ya kupunguza vifo
vya mama na mtoto si jukumu la madaktari au hospitali pekee lakini
jukumu la jamii nzima kukabiliana na huduma hiyo, alisema vyombo vya
habari ikiwemo mitandao ya jamii inakilasababu za kuonesha mapungufu na
kueleza changamoto katika huduma za afya zinazotolewa kwa lengo la
kuboresha zaidi huduma hizo. Alisema tatizo la elimu ya afya ya uzazi ni
kubwa nchini kwani takwimu zinaonesha kwa kila saa moja kuna mama
anayepoteza maisha kutokana na matatizo ya uzaziSerikali. "...Kila siku
kuna akinamama takribani 24 wanapoteza maisha kutokana na matatizo ya
uzazi nchini," alisema Dk. Mwakatundu. Awali akizungumzia hali halisi ya
uzazi wa mpango nchi, Meneja Mawasiliano wa WLF, Victoria Marijani
alisema kuna faida kuwa ya kuzingatia Uzazi wa Mpango kwani ni uwekezaji
wenye faida na endelevu ambao unachangia kupunguza vifo vitokanavyo na
uzazi kwa kiasi kikubwa hadi asilimia 44. Aliongeza kuwa uwekezaji huo
wa ziada katika afya, elimu, usawa wa kijinsia na uwepo wa sera wezeshi
za kiuchumi vitaiwezesha nchi kupata manufaa yatokanayo na ukuaji wa
haraka wa uchumi. Alisema familia zinazotumia uzazi wa mpango zinakuwa
na uwezo wa kuwatimizia watoto mahitaji yao muhimu kama chakula, elimu,
mavazi, huduma za afya na makazi. "...Atapata muda wa kushiriki katika
shughuli za jamii, Atamudu kujiwekea akiba, Atakuwa na amani na upendo
kwa familia yake. Alisema kiwango kikubwa cha vifo vya watoto chini ya
miaka 5 (vifo 81 kwa vizazi hai 1000) Kiwango kidogo cha utumiaji wa
njia za kisasa za uzazi wa mpango (Asilimia 27). Wastani wa utumiaji wa
njia za kisasa za uzazi wa mpango hapa nchini bado ni mdogo. Ni asilimia
27 tu ya wanawake walio kwenye umri wa kuzaa ndio wanaotumia njia za
kisasa za Uzazi wa Mpango.