Balozi wa Ireland nchini Tanzania, Bi. Fionnuala Gilsenan, akitoa
hotuba yake wakati wa maonyesho ya sayansi kwa wanafunzi wa sekondari
yanayoandaliwa na shirika la YST ambayo pia Ubalozi wake unadhamini kila
mwaka.
Na Daniel
Mbega
UBALOZI wa
Ireland nchini Tanzania, umewapatia scholarship Watanzania 14 ili kusoma
kozi
mbalimbali za shahada ya uzamili (masters) na huku wanne kati yao wakienda
kusoma
vyuo vya nje ya nchi hasa University College Dublin, Dublin Institute of
Technology na National University of Ireland Maynooth.
Kwa mujibu
wa taarifa kutoka Ubalozi wa Ireland nchini, scholarship hizo zimetolewa na
ubalozi huo kama sehemu ya Mpango wa Mafunzo wa Kila Mwaka (Fellowship
Training
Programme), ambapo wataalamu wanne waliobahatika kwenda ng’ambo watakwenda
kusomea kozi za Maendeleo Endelevu (Sustainable Development), Kilimo na
Maisha
ya Vijijini (Agriculture and Rural Livelihoods), Rasilimali Watu (Human
Resource Management), na Immunolojia na Afya ya Binadamu (Immunology and
Human
Health).
Watanzania
wengine 10 wamedhaminiwa kusomea kozi mbalimbali katika vyuo vikuu vya hapa
nchini.
Taarifa
hiyo inasema, sherehe za kuwapokea wale walihitimu na kuwakabidhi
scholarship
wale wanaokwenda kuanza, zitafanyika kesho mchana katika ofisi za Ubalozi
zilizoko
Masaki, jijini Dar es Salaam ambapo Balozi wa Ireland nchini, Fionnuala
Gilsenan, ndiye atakayetoa scholarship hizo.
Mpango huo
wa Mafunzo wa kila Mwaka, kwa mujibu wa taarifa hiyo, kwa kiasi kikubwa
unahusisha Mfuko wa Misaada wa Ireland (Irish Aid) kupitia program ya
maendeleo
ya Ubalozi huo nchini Tanzania.
Wanufaika wa
mpango huo wameteuliwa na washirika wa maendeleo wa Ireland nchini Tanzania,
zikiwemo wizara mbalimbali za Serikali, halmashauri za wilaya na mashirika
yasiyo ya kiserikali, ambayo shughuli zao zinawiana na maeneo ya vipaumbele
vya
Irish Aid, hususan Kilimo, Afya, Lishe na Utawala.
Aidha,
wanufaika wote ni watendaji wa kati ambao baada ya kuhitimu masomo yao
watarejea kwenye mashirika na taasisi zao kutumia ujuzi walioupata kwa
manufaa
ya jamii.
“Kwa wanufaika
watakaokwenda kusoma nchini Ireland, program inatoa fursa nzuri ya kujifunza
katika hadhi ya kimataifa na kunufaika na hazina kubwa ya nyenzo za tafiti
zinazotolewa kwenye Vyuo Vikuu na Taasisi za Teknolojia za Ireland,”
imeeleza
taarifa hiyo.
Ikaongeza:
“Inatarajiwa kwamba mafunzo ya wataalamu hawa yatachangia kwa kiasi kikubwa
maendeleo ya Tanzania, na kuendelea kuimarisha ushirika wa kielimu baina ya
Ireland na Tanzania.”
Ireland,
kupitia Mfuko wa Misaada (Irish Aid), imekuwa ikidhamini Mpango huo wa
Mafunzo nchini
Tanzania kwa miaka 40 sasa ambapo program hiyo imekuwa msingi wa msaada
katika
kuzijengea uwezo nchi zinazoendelea na inaendana na mkakati wa kupunguza
umaskini wa nchi washirika wa Ireland, hasa lengo likiwa kuwapatia wataalamu
elimu ya juu ili waendeleze taasisi zao.
Baadhi ya
taasisi washirika zitakazonufaika na mpango wa mwaka huu ni pamoja na
Wizara ya
Kilimo, Chakula na Ushirika, Wizara ya Mifugo na Maendeleo ya Uvuvi,
Halmashauri
ya Wilaya ya Kigoma, Halmashauri ya Wilaya ya Misenyi, Halmashauri ya
Wilaya ya
Kondoa, Halmashauri ya Wilaya ya Muheza, Halmashauri ya Wilaya ya
Ngorongoro, Taasisi
ya Chakula na Lishe, Hospitali ya CCBRT, shirika la Sikika, Mpango wa
Maendeleo
wa Kinapa (Kinnapa Development Programme), shirika la CARE Tanzania na
Taasisi
ya Afya Ifakara (IHI).
(Imeandaliwa
na www.brotherdanny.com/Simu:
0656-331974)
HII HAPA NI TAARIFA KWA VYOMBO VYA
HABARI:
PRESS RELEASE
Fellowship Training Programme
Awards Four Scholarships
to Study in Ireland
Four Tanzanian professionals
have been awarded
scholarships to pursue their post-graduate masters’ degrees in Ireland. The
scholarships were awarded by the Embassy of Ireland in Tanzania as part an
annual Fellowship Training Programme. The fellows will study Sustainable
Development, Agriculture and Rural Livelihoods, Human Resource Management,
and
Immunology and Human Health. A further ten Tanzanians have also been awarded
scholarships to study in Tanzania.
The Fellowship Training
Programme is closely connected
with Irish Aid, the Embassy’s development programme in
Tanzania. The fellows have been nominated by Ireland’s development partners
in
Tanzania, including Government ministries, district councils and
non-governmental organisations, whose work is closely aligned with Irish
Aid’s priority
areas - Agriculture, Health, Nutrition and
Governance.
The fellows are all mid-career
professionals who, on
completion of their studies, are committed to resuming work with their organisations
and putting their
acquired specialist knowledge and skills into practice for the benefit of
the
wider community. For the fellows studying in Ireland, the programme
presents a
unique opportunity to study in an international setting and benefit from the
research facilities provided at Ireland’s Universities and Institutes of
Technology.
It
is anticipated that the training and development of these key individuals
will
contribute to Tanzania’s development, and continue to strengthen the
educational linkages between Ireland and Tanzania.
Notes to the
Editor
· *
Ireland has supported a Fellowship Training
Programme for 40
years. The programme is a key element in support of capacity building in
developing countries and is closely aligned with the poverty reduction
strategies of Ireland’s partner countries. The objective is to strengthen capacity
of partner organisations
through the provision of higher education opportunities.
· *
Irish Aid is the
Irish Government’s programme of overseas development. Irish
Aid has been providing development assistance to Tanzania since
1975.
· *
Partner organisations
benefiting from this year’s fellowship training programme include the Ministry of Agriculture, the
Ministry
of Livestock and Fisheries Development, Kigoma
District
Council,
Muheza District Council, Ngorongoro
District Council, Kondoa District Council,
Missenyi District Council, Tanzania Food and Nutrition Centre, CCBRT, Sikika, Kinnapa
Development Programme, CARE
Tanzania and the Ifakara Health Institute.
· *
The four fellows who will study in Ireland will
attend
University College Dublin, Dublin Institute of Technology and the National
University of Ireland Maynooth respectively.
Embassy
of Ireland
20th
August, 2015
For further information please
contact:
Brian Nolan, Second
Secretary, Embassy of Ireland, Dar es Salaam
Tel: (+255 22) 260 2355 │ Fax:
(+255 22) 260 2362 │ Email: brian.nolan@dfa.ie