Mgombea urais wa Tanzania kupitia Chama
cha ACT-Wazalendo, Anna Mghwira (kushoto), akihutubia katika uzinduzi
wa kampeni ya chama hizo uliofanyika viwanja vya Zakhem Mbagala jijini
Dar es Salaam leo.
Kiongozi Mkuu wa Chama cha ACT-Wazalendo, Kabwe Zitto akihutubia katika uzinduzi huo.
Mshauri wa Chama cha ACT-Wazalendo, Profesa Kitila Mkumbo akihutubia kwenye uzinduzi huo.
Kiongozi Mkuu wa Chama cha ACT-Wazalendo, Kabwe Zitto (kushoto), akiteta jambo na Mgombea urais wa Tanzania kupitia Chama cha ACT-Wazalendo, Anna Mghwira.
Viongozi mbalimbali wa chama hicho wakiimba wimbo wa taifa.
Kiongozi Mkuu wa Chama cha ACT-Wazalendo, Kabwe Zitto, akiwatambulisha wagombea ubunge wa majimbo yote ya Dar es Salaam.
Kiongozi Mkuu wa Chama cha ACT-Wazalendo, Kabwe Zitto, akigawa ilani ya chama hicho kwa mgombea urais na mwenza wake.
Mgombea Mwenza, Hamad Mussa Yusuph akihutubia kwenye uzinduzi huo.
Mwana muziki Bwana misosi, akitoa
burudani katika uzinduzi wa kampeni wa Chama cha ACT-Wazalendo
uliofanyika viwanja vya Zakhem Mbagala Dar es Salaam leo.
Umati wa Wananchi ukiwa katika uzinduzi
wa kampeni wa Chama cha ACT-Wazalendo uliofanyika viwanja vya Zakhem
Magala Dar es Salaam leo.