RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE AHIMIZA UJENZI WA BARABARA ZA VIJIJINI


Raisi Jakaya Kikwete amewataka viongozi wa serikali za mitaa
kuhakikisha kuwa wanajenga barabara maeneo ya vijijini ili kuchochea
maendeleo katika  maeneo ya vijijini na kufungua fursa mbalimbali za
kiuchumi zilizoko katika maeneo hayo.



Kikwete amesema hayo  wakati akihutubia mkutano wa Viongozi wa
serikali za mitaa (TAMISEMI) uliowakutanisha wakuu wa
mikoa,wilaya,Pamoja na Wakurugenzi  kwa lengo la kuimarisha usimamizi
wa ubora wa kazi  na barabara endelevu,Raisi Kikwete amesema kuwa
ujenzi wa barabara vijijini utafungua milango ya maendeleo vijijini na
kubadilisha maisha ya watu wengi



Pia Rais Kikwete amewataka Viongozi wa Serikali za mitaa kuwa
waaminifu katika kusimamia mfuko wa barabara ambao umefikia kiasi cha
shilingi bilioni 800 ili mfuko huo uweze kuwahudumia Watanzania badala
ya kuwanufaisha watu wachache.



“Fedha hizi za mfuko wa barabara zikitumika vizuri zitapunguza
matatizo ya miundombinu ya barabara yanayozibili sehemu nyingi nchini”
Alisema Kikwete





Waziri wa TAMISEMI ,Hawa Ghasia amesema kuwa wizara yake imeanzisha
idara kamili ya Miundombinu ambayo itafanya ukaguzi na kuzuia hasara
inayotokana na ujenzi wa barabara chini ya kiwango.

Ghasia alisema kuwa kumekua na changamoto ya fedha inayokwamisha
ukarabati wa barabara za mitaa ambazo husiadia upanuzi wa miundombinu
katika maeneo mbali mbali.





Katibu Mkuu wa Wizara ya TAMISEMI ,Jumanne Safini  amesema kuwa Wizara
hiyo inakabiliwa na changamoto ya  kukosekana kwa rasilimali za
kutosha  hali inayosababisha viwango duni vya barabara vinavyotokana
na kukosekana kwa usimamizi  na ukaguzi  hivyo kutopata barabara
endelevu.

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

Previous Post Next Post