Ticker

6/recent/ticker-posts

MAUAJI YA KINYAMA YATOKEA ARUSHA ,MTU MMOJA ACHINJWA KAMA KUKU

MAUAJI ya kutisha yametokea  katika hotel ya kitalii ya A. Square Belmont
maarufu kwa jina la A.M iliyopo katikati ya jiji la Arusha,baada ya mtu
asiyefahamika wa jisi ya kiume kukutwa amechinjwa kama kuku na kuondolewa
viungo vyake kikiwemo kichwa ,viganja vya mikono na sehemu za siri.



Tukio hilo la kusikitisha limegundulika leo  majira ya asubuhi  na wahudumu
wa hotel hiyo walipofika katika chumba alichokodi marehemu kwa lengo la
kukifanyia usafi.



Taarifa zinadai kuwa marehemu alifika katika hotel hiyo agost 29 mwaka huu
na kukodi chumba kimoja wapo gorofa ya pili na kulipia siku mbili zaidi
,hata hivyo juzi agost 30 aliongeza siku moja zaidi hadi tarehe agost 31.



Moja wa wahudumu katika hotel hiyo ambaye hakutaka kutaja jina lake alidai
kuwa marehemu wakati anapatiwa chumba hicho alikuwa mwnyewe na kuandikisha
jina moja akidai anatokea wilayani Karatu akifanyakazi ya Ualimu.


“Asubuhi ya leo mhudumu alienda kufanya usafi katika vyumba vya wateja na
walipo fika chumba cha marehemu walijaribu kukifungua na kukikuta kiko wazi
na walipo jaribu kuingia ndani ya chumba hicho ndipo walipoona mwili wa
marehemu ukiwa utupu umelazwa kifudi fudi katika bafu la chumba hicho huku
michirizi ya damu ikiwa pembeni ” alisema mhudumu huyo.



Aidha kufuatia tukio hilo uongozi wa hotel ulitoa taarifa kituo cha polisi
na polisi walifika na kuchukua mwili huo hadi chumba cha kuifadhia maiti
kilichopo hospitali ya mkoa Mount Meru .



Hata hivyo kabla ya kuchukuliwa mwili huo , polisi walitumia masaa matano
kuwahoji wahudumu wa hotel hiyo  kufanya uchunguzi wa kina zaidi kuhusiana
na tukio hilo

Uongozi wa hotel hiyo haukuwa tayari kuzungumzia tukio hilo na muda mwingi
walionekana  kujifungia katika vyumba maalum kukwepa waandishi wa habari


Kamanda wa polisi mkoa wa Arusha Liberatusi Sabasi alithibitisha tukio hilo
na kueleza kuwa atalitolea ufafanuzi hapo baadae,


Tukio hilo linahusishwa na ushirikina na hakuna anayeshikiliwan kuhusiana
na tukio hilo na kwamba baada ya mauaji hayo wauaji waliondoka na nguo za
marehemu pamoja na viungo vyake kikiwemo kichwa.
habari kwa hisani ya libeneke la kaskazini blog

Post a Comment

0 Comments