MGOMBEA ubunge jimbo la Arusha mjini kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi
,Philemon Mollel maarufu kama Monaban amewaahidi wananchi wa jiji la
Arusha kuwaletea mabadiliko baada ya kumpitisha katika kura za maoni
kupeperusha bendera ya chama hicho jijini Arusha.
Aliyasema mara baada ya kutangazwa rasmi na Mkurugenzi wa
tume ya taifa ya uchaguzi ,Juma Iddi kuwa mgombea wa ubunge jimbo
hilo baada jina lake kupitishwa na Halmashauri Kuu ya Chama cha
Mapinduzi (NEC) ,kuipeperusha bendera ya ccm na hivyo kuwataka
wananchi kuendelea kuungana naye katika kuhakikisha ifikapo oktoba 25
wanampa kura za ndio .
Mlollel alisema kuwa, kwa muda mrefu sasa jimbo la Arusha limekosa
kiongozi aliye makini na mwenye kujali kero na changamoto za wananchi
na badala yake walikuwa na bora kiongozi na sio kiongozi bora.
Alisema kuwa, atahakikisha ahadi zote alizozitoa kwa wananchi wa jimbo
la Arusha zinatekelezwa zote hasa katika upande wa uchumi ambao
umekuwa mbovu kutokana wa kukosekana amani kwa muda mrefu na
kusababisha watalii kutofika kwa wingi .
'kwa kweli wananchi watarajie neema sasa imebaki kazi kwao tu
kunichagua mimi oktoba 25 ili niweze kutimiza malengo yote niliyoahidi
ambayo nitahakikisha nayatekeleza kwa kushirikiana na viongozi wa
ngazi mbalimbali kuanzia ngazi za vijiji,kata na hata mkoa kwani
shughuli zozote za maendeleo siku zote zinahitaji ushirikiano mkubwa
sana'alisema Mollel.
Alisema kuwa,kitendo cha wananchi wa jiji la Arusha kumkopesha imani
yeye kinaonyesha dhahiri jinsi ambavyo wananchi wamechoka na
maandamano pamoja na vurugu zisizoisha kila wakati na hivyo
atahakikisha hayo yote yanakomeshwa na kuwashangaza wananchi wa jiji
la Arusha.
Mollel alisema kuwa,kilichokuwa kimekosekana kwa wananchi wa jiji la
Arusha kwa muda mrefu ni kiongozi asiyekuwa na ushirikiano na wananchi
wake jambo ambalo limekuwa likichangia kuwepo kwa vurugu na machafuko
,hivyo wananchi kwa sasa wamechagua jibu sahihi la jimbo la Arusha
mjini.
Alisema kuwa, katika kusaka nafasi hiyo ya ubunge walijitokeza
wagombea 14 ambao ni wa Chama cha Mapinduzi ambapo baadhi yao
wamefurahia uteuzi huo uliopitishwa na Halmashauri kuu ya Chama cha
Mapinduzi (NEC) na ana waahidi kuzidisha ushirikiano huo lengo moja
likiwa ni kuhakikisha kuwa jimbo la Arusha linarudi mikononi mwa CCM.