Selemani Rashidi, Namba
msaada kwa yeyote anisaidie niweze kufanyiwa matibabu kwa
kinyama kilicho jitokeza kichwani mwangu toka nilipo
zaliwa.
Selemani Rashidi, anapoishi na
mama yake mzazi
Selemani Rashidi (kushoto), akiwa na
mama yake mzazi pichani, ambaye alisimulia mkasa mzima wa mwanaye,
alizaliwa akiwa mzima na baada ya kuzaliwa alipatwa na matatizo ya
ugonjwa wa Degedege na alimpeleka kwa mganga wa kienyeji na kupona
matatizo hayo na ndipo kikaota kipele kichwani cheusi na kikawa
kinakuwa na kushikana na sikio, kutokuwa na uwezo wa kipesa hakuweza
mpeleka popote, Baba yake yapata Miaka kumi na tano toka afariki na
ukizingatia ni pesa inayo hitajika, hayo yalisemwa na mama yake mzazi
ambaye anaitwa Zamda Kibosha, wakiwa wamekaa kwao maeneo ya
kitongoji cha Lugongoni, (A) Kataa ya Nguruka Wilaya ya
Uvinza Mkoa wa Kigoma, Mama yake anasema mwanaye baada ya kuota
kinyama hicho, kauli kutoka ni kwa shida, akijibu maramoja harudii
tena kuongea na chooni anakwenda mwenyewe na kula anakula kama
kawaida, mama anaomba kwa mtu yoyote mwenye kuona na kusia anaomba
msaada wa hali na mali ili mwanaye apate matibabu, kwa mawasiliano
mwenye chochote kitumwe kwenye namba 0687946492, Mariam Hamza Thabiti,
Nguruka kigoma. (PICHA ZOTE NA KHAMISI MUSSA) Mmiliki wa ujijirahaa
blo.