vifaa vipya vya kisasa vya kupima mwendo
wa magari,Vifaa vinauwezo wa kurekodi mwendo wa gari na wakati huo huo
kuchukua picha ya mnato au video ya gari husika.
Ili kuongeza ufanisi wa
vifaa hivi, tumeelekeza askari wanaoshika vifaa hivyo wasivae sare ili
wakishapata mwendo na picha za magari yaliyokiuka mwendo watoe taarifa
kwa wenzao wenye sare wafanye ukamataji.
Akiongea na waandishi wa habari KAMANDA WA POLISI,
KIKOSI CHA USALAMA BARABARANI (T) MOHAMMED R.MPINGA alisema kuwa Utaratibu huu unasaidia kuondoa dhana ya askari kujificha na kusimamisha magari kwa kushtukiza na kwa upande mwingine itapunguza tabia ya madereva kupeana ishara kuonyesha mahali walipo askari.
KIKOSI CHA USALAMA BARABARANI (T) MOHAMMED R.MPINGA alisema kuwa Utaratibu huu unasaidia kuondoa dhana ya askari kujificha na kusimamisha magari kwa kushtukiza na kwa upande mwingine itapunguza tabia ya madereva kupeana ishara kuonyesha mahali walipo askari.
Jeshi la Polisi linawakumbusha Madereva na watumiaji wote wa barabara kuziheshimu sheria na kanuni za usalama barabarani.
"Aidha nachukua
nafasi hii kuwakumbusha askari wote kusimamia sheria na kanuni za
usalama barabarani bila woga au upendeleo kwa kuzingatia maadili mema ya
kazi".
Alisema kuwa anawajulisha watumiaji wote wa barabara hususani
madereva kuwa askari wataendelea kuwa wakali sana katika kipindi hiki
kwa kusimamia sheria kikamilifu ambapo hatua kali za kisheria
zitachuliwa kwa yeyote atakayekamatwa akivunja sheria za usalama
barabarani.
Ndugu wanahabari,
Ndugu wanahabari,
wakati huo huo aliwaasa wananchi na wadau wa usalama barabarani kwa ujumla, watoe ushirikiano zaidi kwa kutoa taarifa za uhalifu wa usalama barabarani, kufuata sheria, kanuni na maelekezo kwa ajili ya usalama wao watumiapo barabara.
Kila mmoja atambue haki na wajibu wake awapo barabarani ikiwa ni kuwa na subira na kujali watumiaji wengine wa barabara kwani kila mmoja anayo haki sawa ya kutumia barabara. Watoto wasiachwe kutembea barabarani bila ya uangalizi wa watu wazima.
ENDESHA SALAMA - OKOA MAISHA.
Imetolewa na:
MOHAMMED R.MPINGA – DCP,