Mgombea mwenza wa CCM, Bi. Samia Suluhu akiwa
jukwaani akinadi ilani ya Chama Cha Mapinduzi Jimbo la
Iramba
Magharibi, Mwigulu Nchemba Mjumbe wa Kamati ya Kampeni
Taifa, Mwigulu Nchemba ambaye pia ni mgombea wa ubunge Jimbo la Iramba
Magharibi akizungumza na wananchi kuinadi ilani ya CCM Baadhi ya wanaCCM na
wananchi wakiwa katika mkutano wa kampeni wa mgombea mwenza wa Chama Cha
Mapinduzi (CCM) uliofanyika katika Jimbo la Iramba Magharibi Mbunge Nkenge CCM aliyemaliza muda
wake, Asumpta Mshana akiinadi ilaya ya CCM Helkopta ya mgombea ubunge wa Jimbo la Singida
Kaskazini ikitu Mgombea ubunge wa Jimbo la Singida Kaskazini anayeomba kuchaguliwa tena,
Lazaro Nyarandu akiwarudisha baadhi ya wananchi kurudi eneo la Mkutano wa
kampeni na kuacha kushangaa helkopta. Mgombea
ubunge wa Jimbo la Singida Kaskazini anayeomba kuchaguliwa tena, Lazaro
Nyarandu akielekea eneo la mkutano pamoja na baadhi ya wananchi baada ya
kutua na helkopta. Helkopta iliyomshusha gombea ubunge wa Jimbo la Singida
Kaskazini anayeomba kuchaguliwa tena, Lazaro Nyarandu ikiwa
inamsubiri. Mjumbe wa Kamati ya Kampeni Taifa, Mwigulu
Nchemba (kushoto) wakimpongezana Katibu wa CCM Mkoa, Merry Mziku jimboni
Iramba Magharibi Bi. Suluhu kulia akizungumza neno na Mwigulu Nchemba na Bi.
Mziku Mjumbe wa Kamati ya Kampeni
Taifa, Mwigulu Nchemba ambaye pia ni mgombea wa ubunge Jimbo la Iramba
Magharibi akizungumza na wananchi kuinadi ilani ya CCM.[
Baadhi ya wanaCCM na wananchi wakiwa katika mkutano wa kampeni wa mgombea
mwenza wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mjumbe wa Kamati ya Kampeni
Taifa, Mwigulu Nchemba ambaye pia ni mgombea wa ubunge Jimbo la Iramba
Magharibi akizungumza na wananchi kuinadi ilani ya CCM Burudani kidogo kabla ya ilani kuendelea
kunadiwa jimboni Iramba.
Na Joachim Mushi, Singida
MGOMBEA ubunge wa Jimbo la Singida Kaskazini anayeomba
kuchaguliwa tena, Lazaro Nyarandu amenogesha kampeni za mgombea mwenza wa
Chama Cha Mapinduzi CCM, Bi. Samia Suluhu katika mikutano yake inayoendelea
ya kuinadi ilani ya CCM.
Nyarandu ambaye jana alishuka kwa helkopta ya kukodi Jimboni kwake ikiwa ni
muda mfupi baada ya mkutano wa kampeni kuanza alivuta hisia za wanaCCM na
wananchi katika mkutano huo. Kama hiyo haitoshi mgombea huyo wa ubunge
alitumia helkopta hiyo kwenye mikutano ya kampeni za mgombea mwenza ya
Jimbo la Iramba Magharibi.
Akihutubia mkutano wa kampeni katika Kata ya Kengege, Jimbo la Iramba
Magharibi mkoani Singida, Bi. Suluhu aliwaomba wananchi kuipigia kura CCM
kwani ndani ya ilani yake imepanga kufanya mambo mazuri kwa maendeleo ya
mkoa huo. Alisema endapo watachanguliwa watajenga kiwanda kikubwa cha
kusafishia mafuta ya alizeti jambo ambalo litaongeza thamani ya mazao kwa
wakulima wa eneo hilo.
Aliongeza kuwa mbali na kiwanda hicho kikubwa kuwanufaisha wakulima pia
kitatoa nafasi za ajira kwa vijana ambapo jumla ya wafanyakazi 600 watapata
ajira ndani ya kiwanda hicho, alisema baada ya Serikali ya awamu ya nne
kujenga shule za Sekondari za kata za kutosha na maabara ilani mpya ya CCM
imepanga kushughulikia suala la vifaa vya maabara hizo ili ziweze kutumika
kwa ufasaha.
Bi. Suluhu alisema Mkoani Singida imepanga kujenga hospitali kubwa ya rufaa
ambayo itakuwa ikitoa huduma katika mkoa huo na mikoa ya jirani, pamoja na
ujenzi wa barabara ya Ndago.
Aidha akihutubia katika Mkutano mwingine Wilaya ya Ikungi aliahidi kufanya
jitihada za ujenzi wa hospitali ya Wilaya ya Ikungi ili kusongeza huduma
kubwa za afya kwa wanaIkungi, pamoja na kuvipatia umeme vijiji ambavyo bado
havijafikiwa na huduma hiyo kupitia mradi wa Wakala wa Umeme Vijijini (REA)
awamu ya pili.
Aliongeza kuwa licha ya maeneo ya mikoa ya singida kukabiliwa na tishio la
ukame aliwahakikishia hakuna raia atakayekufa njaa katika maeneo hayo.
"...Serikali imejipanga na ghala la kuhifadhi chakula lina akiba ya
kutosha, hivyo niwahakikishie hakuna mwanakijiji ambae atakufa kwa njaa.
Kwa upande wake Mjumbe wa Kamati ya Kampeni Taifa, Mwigulu Nchemba ambaye
pia ni mgombea wa ubunge Jimbo la Iramba Magharibi akizungumza jimboni hapo
alisema ilani ya CCM imepanga kutekeleza miradi ya maji katika Vijiji vya
Mgundu, Kinampanda, Makunda pamoja na vijiji vingine vinavyokabiliwa na
kero ya maji.
Alisema baadha ya mradi wa ujenzi wa shule za Sekondari za kata kufanikiwa
serikali itakayoundwa na CCM imepanga kusimamia ujenzi wa mabweni ili
kuwanusuru watoto wanaotembea umbali urefu kwenda shuleni pamoja huku
wasichana wakikabiliwa na changamoto za kubebeshwa mimba na kukatishwa
masomo yao.
Mwingulu aliwataka wananchi kutochagua vyama vingine kwani havina hoja za
msingi na vingine vinaazima hadi wagombea ili viweze kuwasimamisha. Bi.
Suluhu anaendelea na ziara yake ambapo sasa anaelekea Mkoa wa Dodoma
akiinadi ilani ya CCM.