WALIMU ARUSHA WAIDAI SERIKALI BILIONI 4

Mwenyekiti wa Chama cha Walimu mkoa wa Arusha ,Mwalimu Jovin  Kuyenga
akizungumza na waandishi wa habari jana Ofisini kwake  juu ya deni la
shilingi bilioni 4 wanalodai  kwa serikali,kushoto ni Katibu wa Chama cha
Walimu mkoa wa Arusha, Mwalimu Hassan Saidi.

Chama cha Walimu mkoa wa Arusha CWT wamelalamikia serikali na kuitaka
kutekeleza kwa wakati madeni yao la zaidi ya billioni 4 kwani yamekuwa
kikwazo katika ufanisi wa kazi hali ambayo inapelekea walimu wengi
kushindwa kuendelea kufanya kazi kwa moyo na kujituma jambo ambalo linaweza
kushusha kiwango cha elimu nchini.



Akizungumza na Waandishi wa habari, Mwenyekiti wa chama cha walimu mkoa wa
Arusha Mwalimu Juvin Kuyenga amesema, kumekuwa na chanagamoto kubwa ambazo
zinakwamisha ufanisi wa kazi kwa walimu kwani wanazidai halmashauri
zilizopo mkoani zarusha zaidi ya billioni nne ,amabapo katika jiji la
arusha wanadai millioni  987,689,00,Arumeru billioni
2,996,607,848.21,Karatu  millioni 423,983,820,Longido millioni 171,112,680,
Ngorongoro million 169,000,000, na Monduli 135,832,000.



Mwalimu Kuyenga ameendelea kusema kuwa,madeni haya yanatokana na madai
mbalimbali ikiwa ni pamoja na malimbikizo ya mishahara
,mafunzo,uhamisho,matibabu na likizo pamoja na mapunjo ya mshahara na
madeni haya yamekuwa ni kero kubwa  na kusababisha wakati mwingine walimu
kuzichukia kazi zao.



Alisema kuwa Walimu wamekuwa wakigota madaraja bila kupanda kwa muda mrefu
kati ya walimu 12,319 waliopo mkoani arusha walimu 5,364 wamegota kwenye
madaraja yao na bado hawajafunguliwa  pamoja na serikali ilishatoa waraka
wa kufungua madaraja tangu julai 2014 hivyo wametaka seriakali kuhakikisha
inapandisha madaraja kwa wakati.



‘Posho ya madaraka kwa viongozi wa elimu, wakuu wa shule,wakuu wa vyuo
kutokana na waraka wa seriakali uliotolewa mwaka jana posho hiyo alitakiwa
ianze kutolewa kuanzia julai mwaka huu 2015 lakini hadi sasa bado pesa hiyo
haijanza kutolewa hii inakuwa kama danganya toto kwa viongozi wetu” alisema
mwalimu Juvin Kuyenga.



Hivyo  wameilalamikia serikali juu ya kuchelewesha kwa malipo kwa wastaafu,
sababu kuna walimuwaliostaafu toka january  zaidi ya walimu 67 huku
wakiishi katika mateso ilihali wameshastaafu kazi na mpaka leo hawajapata
viiinua mgongo vyao



 “Tunaidai serikali sababu tunapowasiliana na hawa wa mifuko ya hifadhi za
jamii inasema serikali bado haijawarejesha michango ya walimu inayotakiwa
kupelekwa hivyo na danadana hizi zinawafanya walimu kuona haki zao
zinanyonywa kwani utasababisha ufanisi kuwa mdogo makazini” Alisema



Sababui swala hili laweza kupelekea malumbano kati ya walimu na serikali
ukizingatia katika kipindi cha kueleka katika uchaguzi ,mitihani ya darasa
la saba na kidato cha nne kwani kukataa huku tamaa kunaweza kupelekea vitu
hivyo vya taifa kushindwa kufanikiwa.



Kwa upande wake Katibu wa Chama cha Walimu mkoa wa Arusha, Mwalimu Hassan
Saidi amesema chama hicho kimetoa wiki mbili kwa  waajiri wa halmashauri
zilizopo mkoa wa arusha kuwarudisha majumbani walimu waliostaafu na
wanaostaafu na wasipofanya hivyo watawachukulia hatua za kisheria ikiwa ni
pamoja na kuwashtaki mahakamani kwani wamekuwa wakiteseka sana baada ya
kustaafu na ni kinyume cha sheria .



Mwalimu Saidi , amewataka wagombea wa Uraisi kutazama vipaumbele vya walimu
walivyovitoa likiwemo la kuwapatia walimu  kompyuta mpakato (laptop)  wakati
wanamahitaji mengi na ya  msingi zaidi ya hayo ikiwa ni pamoja na mishahara
isiyokidhi mahitaji ya walimu na kurejeshwa na kwa posho ya kufundishia kwa
walimu.


Kwa taarifa tulizozipata kutoka kwa vyanzo vyetu kuwa baraza la kuu la
walimu tanzania  wanatarajiwa kukutani mkoani dodoma  Agosti  31 hadi
Septemba 8 mwaka huu kwa ajili ya kutoa matamko ya kitaifa juu ya kero hizi
nyingi wanazozipata walimu


 

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

Previous Post Next Post