TIMU 14 ARUMERU ZACHUANA KUWANIA KOMBE LA SETH BENJAMINI

Jumla ya timu  14 kutoka wilaya ya Arumeru, Mkoani Arusha ,zinachuana vikali katika mashindano ya soka  kuwania kombe la SETHBENJAMINI aliyekuwa muasisi wa Azimio laArusha ambaye alifariki mwaka  1967.
Timu hizo ni  ST.Domingo , Manyata, Duluti,Rafiki, Railway sports club, Maji ya chai, Embaseni,Usa Star,Meru Worrious, Pande za home Chemchem, Magadini ,Waya mkali na Chackyi SC zinachuana vikali katika mashindano hayo yanayofanyika katika viwanja vya Ngaresero .
Kwa mara ya kwanza  mashindano hayo kufanyika ili kuweza kumkumbuka mwasisi huyo ambaye  anakumbukwa kama shujaa ,alikuwa akisafiri kutoka Arusha kwa matembezi  kuelekea Dar es salaam ambapo  alipofika eneo la maji ya chai ,Usa river alizidiwa gafla na kupoteza maisha papo hapo ilikuwa mwezi julai mwaka 1967 , kwa mujibu wa diwani wa kata ya Usa River  (CCM) Zubery Simbano.
Simbano alieleza kuwa wameamua kushirikiana na familia ya marehemu ili kuweza kumuenzi  katika soka akiwa yeye ni mmoja wa mashujaa ambao inaonekana wamesahaulika ,hivyo wataendelea kumuenzi na kumkumbuka kila mwaka .
“ Mashindano haya  yalianzatarehe  22 Julai na tunataraji yatamalizika   tarehe 5 septemba mwaka huu ambapo yata hitimishwa  na maandamano kutoka mahali alipozikwa muasisi huyo, eneo la Laki tatu kanisani hadi  eneo la uwanja wa Ngaresero na maandamano hayo yatahusiha  washiriki wote wa mashindano  pamoja na viongozi wa chama cha mapinduzi (CCM) na Viongozi wa  serikali.”alisema Simbano.
Mshindi wa kwanza ataweza kujinyakulia kitita cha shilingi  laki tano (500,000/=) pamoja na  kikombe  lenye thamani ya shilingi laki  mbili na medali,huku mshindi wa pili atajipatia seti ya jezi  na mipira  miwili sambamba na medali,na mshindi wa tatu atapata mipira 3 na medali.


Pia washiriki wote wataweza kujipatia vyeti ,na kutakuwa na zawadi mbalimbali kwa mfungaji bora, mchezaji bora na timu yenye nidhamu vile vile mwisho wa mashindano kutakuwa na michezo mbalimbali ikiwamo  mbio za baiskeli za km 40 zitakazo anzia katika uwanja wa ngaresero hadi Raundi ya Impala na zitapitia  barabara ya Nelson Mandela,kukimbiza kuku, kuvuta kamba .

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

Previous Post Next Post