MATOKEO YALIYOMPA USHINDI MBUNGE PROF MSOLA KATA TATU YATUPWA ,UCHAGUZI KURUDIA KESHO TAKUKURU WAANZA KUCHUNGUZA MCHAKATO MZIMA KILOLO



Mbunge  wa Kilolo  anayemaliza muda wake Prof  Peter Msolla (katikati) akiwa na  wabunge  wa zamani  ,Stevin Mwabuma( kulia) ambae alikuwa mbunge wa kwanza wa jimbo la Kilolo  na Venance Mwamoto aliyeongoza  jimbo hilo mwaka 2000-2005
.........................................................................................................................................
Na MatukiodaimaBlog
CHAMA Cha mapinduzi ( CCM) mkoa  wa Iringa  kimefuta matokeo ya kata tatu za jimbo la Kilolo matokeo yaliyokuwa yakimpa ushindi mkubwa mbunge anaemaliza muda wake Prof Peter Msola na kuagiza uchaguzi   huo  kurudiwa kesho

Matokeo hayo ambayo yamekataliwa na wagombea wote yanadaiwa kupachikwa katika  vituo vya kata hizo tatu japo hata hivyo hayana uhalisia ukilinganisha na idadi ya wanachama wa maeneo husika .

Katibu  wa CCM  mkoa  wa  Iringa Bw  Hassan Mtenga  alisema  kuwa  kutokana na dosari mbali mbali ambazo  zilijitokeza katika kata  hiyo  ambazo ni Nyalumbu , Lugalo na Uhambingeto  alisema  kilichoonyeshwa ni matokeo hayo kuwa  tofauti na matokeo  halisi ambayo mawakala wa  wagombea  walikuwa nayo na katika kata   hiyo makatibu matawi  na kata  wa CCM hahakuweza kupeleka matokeo kwa wakati kwa  msimamizi  mkuu wa  uchaguzi hadi  alipoyafuata na  kuona kasoro  hiyo .

Katibu   huyo  alisema karatasi  zilizoonyesha ushindi  wa mgombea  mmoja Prof Msolla zilikuwa ni tofauti na karatasi  halisi  zilizotolewa na chama   hivyo kutokana na utofauti  huo  wagombea  wengine  waliweza  kugomea matokeo hayo .


Hata  hivyo mgombea Francis Mkokwa alisema kuwa  walishangazwa kuona ghafla mbunge Prof Msola akiongoza katika vituo vya kata hizo ambazo hata matokeo Yake hayakusainiwa na mawakala wa wagombea wengine na ndizo kata ambazo matokeo Yake yalikuwa na utata na  wakati wa kampeni mbunge   huyo alikuwa hakubaliki katika maeneo ya kata  hizo .

Kwani walisema kimsingi matokeo halali ya kata zaidi ya  21 Mwamoto ndie alikuwa akiongoza kwa kura nyingi zaidi kuliko za mgombea mwingine yeyote huku mbunge anaemaliza muda wake akimfukuza kwa mbali  na  ajabu  kushangazwa  kuona udanganyifu  mkubwa katika kura  hizo.

Bila kutaja matokeo hayo alisema walitegemea matokeo ya jumla Mshindi kuwa Mwamoto ila ilitaka kuwa tofauti kwa ambae hakuongoza ktk vituo kutaka kuongoza kwa matokeo ya jumla hivyo kulazimika kuchunguza matokeo hayo na kubaini Wizi huo .

Kwani katika  vituo idadi ya kura ni nyingi kuliko ile ya wanachama na wakazi wa eneo husika hata kama wana kijiji wote hadi watoto wa mwaka mmoja wangepiga kura bado kura zilikuwa nyingi  kuliko wakazi wa eneo husika kuwa kosa walilolifanya ni kuongeza idadi ya kura za mbunge Prof Msola bila kufuta idadi ya kura za Mwamoto ama idadi ya wapiga kura ya jumla 

"ukitazama idadi halisi ya wapiga kura ,kura zilizopigwa na kura zilizoharibika bado ni vitu viwili tofauti na kufananisha Wizi huo ni sawa na Wizi bila mahesabu ....lazima  chama  kuchukua hatua kali kwa katibu  wa chama  wilaya na wote  waliohusika "

.Mgombea   huyo  alisema  mbali ya kuwa  yeye ni mgombea  bado kwa  sasa   wameamua  kuungana  kupinga wizi   huo na kuona mshindi  wa  kweli anapatikana na  sio udanganyifu  huo ambao  umefanyika.

Kwa  upande  wake  mgombea  Ashrafu  Chusi  pia  alisema katika kata  hizo  kumefanyika  udanganyifu  mkubwa na  kuwa kuna mazingira ya  rushwa  yalifanyika  usiku  wa kuamkia siku ya  kupiga  kura kwa eneo hilo la mji wa Ilula lenye shida kubwa ya maji watu  kupewa  rushwa na  huduma ya maji kwa  kufungulia bomba za maji kwa kituo kimoja baada ya  kingine na  katika  vituo  hivyo inasemekana  walikuwa  wakigawa pia kanga na pesa na pale  mbinu  hiyo  inapobainika  walikuwa  wakifunga maji kituo husika na kufungua kituo cha pili.

Bw  Chusi  alisema  jambo  hilo  wanaomba vyombo  husika kuweza  kuchunguza  zaidi ili  kuwachukulia hatua wahusika na  kuwa hana  shaka hata  kidogo  kuwa mshindi wao katika mchakato  alikuwa ni Mwamoto.

Mwenyekiti  wa  CCM kata ya Nyalumbu  Bw  Bruan Mbululo  alisema  kuwa kimsingi  wao  walikamilisha  kazi yao  kwa  kwenda  kukabidhi matokeo kwa katibu wa CCM wilaya ya  Kilolo na kama kuna dalili  za udanganyifu  wao  hawahusiki japo  alisema katika kata  yake Prof Msola alishinda ila hakumbuki ni kwa  kura  ngapi.

Kamanda  wa taasisi ya  kuzuia na kuopambana na rushwa mkoa  wa Iringa Yunith Mmari  akizungumza na mwandishi wa habari  hizi kwa njia ya  simu  alisema  kuwa wanaendelea  kuchunguza mchakato  huo wa  kura za maoni katika kata  hizo  tatu  za  jimbo la Kilolo.

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

Previous Post Next Post