Ticker

6/recent/ticker-posts

MKUU WA MKOA WA ARUSHA FELIX NTIBENDA KUWA MGENI RASMI KATIKA TAMASHA LA 10 LA VYOMBO VYA HABARI


Katibu wa chama cha waandishi wa habari za michezo na burudani mkoa wa Arusha,(TASWA- Arusha) Mussa Juma
Na Woinde Shizza,Arusha
Mkuu wa mkoa wa Arusha, Felix Ntibenda,anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika tamasha la 10 la vyombo vya habari  vya mkoa wa Arusha. ambalo litafanyika Agosti 29 katika uwanja wa sheikh Amri Abeid.


Akizungumza na waandishi wa habari Palace hoteli jana  mwenyekiti wa TASWA mkoa wa Arusha, Jamila Omar  na Katibu wa TASWA Arusha,  Mussa Juma walisema maandalizi yote muhimu yamekamilika ikiwepo ujio wa timu ya TASWA kutoka jijini Dar es Salaam.
Omar alisema Kauli mbiu ya Mwaka huu ya Tamasha hilo ni kuwa,Uchaguzi bila vurugu inawezekana na   timu zitachuana katika michezo ya Soka, mbio zamagunia, kuvuta kamba, kukimbiza kuku na mpira wa pete.
Alisema mdhamini Mkuu wa Tamasha hilo ni Kampuni ya Bia nchini(TBL), ambapo wadhamini wengine ni TANAPA, Faidika, Mega Trade Investment,na SBC(T) Ltd.
Omar aliwataja wadhamini wengine kuwa ni, Shilika na nyumba nchini(NHC), Kampuni ya Tanzanite One,Coca cola na Big Expedition.
Akizungumzia tamasha hilo, Afisa matukio ya TBL Arusha, Chris Sarakana aliwataka wanahabari na wakazi wa mkoa wa Arusha kujitokeza na kuahidi TBL itaendelea kushirikiana na wanahabari.

Awali Katibu wa TASWA mkoa wa Arusha,Mussa Juma alitaja timu nyingine zitakazoshiriki ni TASWA Arusha, AJTC. Habari Maalum,Radio 5, Radio ,Faidika,Mj radio, Arusha one na ORS kutoka mkoa wa Manyara.
 Alisema kabla ya Tamasha wanahabari watatembelea hifadhi ya Taifa ya Arusha vile vile  kiwanda cha Bia nchini(TBL) mkoa wa Arusha na viwanda vya Mega Trade na Pepsi  mkoani hapa ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 10 ya bonanza hilo

Post a Comment

0 Comments