Afisa kilimo daraja la kwanza wa halmashauri ya mbulu Peter Sangawe akiwa
anaomuonyesha Mkuu wa mkoa wa Manyara Dk Joel Bendera jinsi ya kuifadhi nafaka bila kutumia kemikali
|
Mkuu wa mkoa wa Manyara Dk Joel Bendera akiwa anakagua vitunguu vinavyolimwa na halimashauri ya mbulu
Mkurugeniz wa kampuni ya SaBSAI pangani Enterprises Mr Feroz Kassam akiwa anawaonyesha wananchi waliotembelea katika shamba darasa lao kuangalia Bontera mbolea au dawa ambayo inatumika kuoteshea mazao ili kuwweza kurutubisha aridhi ili mkulima aweze kunufaika,Aidha alisema kuwa mbolea hii au dawa hiii inaweza kumpunguzia mkulima garama mbalimbali huku akitolea mfano kuwa mbolea hii inasaidia kufukuza wadudu ambao wanaweza kushambumazao yakiwa shambani |
wananchi wakiwa wanashangaa tangawizi ambayo inalimwa na halmashauri ya Same
Na Woinde Shizza,Arusha
Wakulima pamaja na wafugaji
wametakiwa kufuata ushauri wa wataalamu
pamoja na kufanyia kazi mafunzo wanayopata kutoka kwa wataalam ili waweze kulima kilimo chenye tija
Hayo yamebainishwa na mkuu wa mkoa wa
Manyara Dk Joel Bendera wakati akitembelea
baadhi ya mabanda yaliyokuwepo katika maonyesho ya nane nane yanayoendelea katika viwanja vya Taso njiro
jijini Arusha.
Alisema kuwa
kumekuwa na tatizo la wakulima wengi kutofanyia kazi elimu wanaopewa kwani wakulima wengi ambao wanapewa elimu
wamekuwa wakichukuwa elimu izo na kuzikalia badala ya kuzifanyia kazi.
Alibainisha
kuwa alitegemea wakulima wa kubwa ambao
wanapata mafunzo haswa katika kipindi cha msimu wa maonyesho ya kilimo nane nane wangeweza kuchukuwa elimu hiyo na kuenda
kuwafundisha wakulima wadogo ambao walishindwa kufika katika maonyesho hayo na
kupata elimu badala yake wakulima hao wamekuwa wakipata mafunzo na kuyaweka
bila kuwagawia wenzio.
“nchi
hii tuna rasilimali nyingi kwakweli tukiangalia maziwa ,mito na mabonde kama
kweli wananchi wetu hususa ni hawa wakulima wangekuwa wanafanyia kazi mafunzo
ambayo wanapewa naimaini tungekuwa mbali kiuchumi kwa kupitia kilimo na ufugaji
pia ajira zingepatikana na sio hivyo tu lakini ata tatizo la njaa kwa ajapa
nchini kwetu lingekuwa ni historia tu lisingetukuta”alisema Bendera
Aidha
alisema kuwa pamoja kuwa kunachangamoto kubwa ya hali ya hewa katika kipindi
hichi lakini iwapo wananchi wangekuwa wanafaaata elimu ya wataalam wanayopewa
wangekuwa wananufaika kwani wangewezakufanya kitu kulingana na hali ya hewa
inavyokwenda akitolea mfano iwapo kama mkulima kabla ya kupanda mbegu angekuwa
anaenda kutafuta ushauri kwa mtaalam basi kama ni maindi anaotesha basi
angeshauriwa ni mbegu gani ingeweza kumfaa kwakipindi hicho.
Aidha
alitoa kwa kulima kuchagua viongozi wanao faa kama vile kauli mbiu ya sasa
inavyosema Matokeo makubwa sasa tuchague viongozi bora kwa maendeleo ya kilimo na ufugaji