Mwenyekiti wa chadema mkoa ambaye pia ni katibu wa taifa wa chadema kanda ya kaskazini akiongea na waandishi wa habari hii leo ndani ya ofisi za chama hicho kanda zilizopo ndani ya jiji la Arusha
waandishi wa habari wakiwa wanasubiri mkutano wa chadema uanze
naibu meye wa jiji la Arusha Prosper Msofe akiwa anafafanua jambo mbele ya waandishi wa habari
Mwenyekiti wa Chadema Kanda ya Kaskazini, Amani Golugwa, amesema
wanaotaka kutangaza nia ya kuwania ubunge katika majimbo ambayo tayari
yana wabunge wa chama hicho, wanatakiwa kusubiri hadi Bunge
litakapovunjwa Julai 2, mwaka huu, ili kuwapa wabunge waliopo nafasi ya
utulivu kufanya kazi za kibunge.
Alisema hadi sasa hakuna mgombea wa kiti cha ubunge Jimbo la
Arusha, ambaye ameandika rasmi barua ya kuelezea nia yake ya kugombea
ubunge katika jimbo hilo.
Alisema kwa mujibu wa utaratibu waliojiwekea, Ofisi ya Kanda ndiyo
yenye jukumu na wajibu wa kuratibu mchakato wa kupokea barua rasmi
pamoja na wasifu wa wagombea.
Hata hivyo, alisema mbunge wa sasa, Godbless Lema ameonyesha nia ya kuendelea kugombea tena kiti chake.
Alisema utaratibu waliojiwekea kwa majimbo ambayo yana wabunge wa
chama hicho, ni kwa wagombea wanaotaka kutangaza nia kusubiri hadi bunge
litakapovunjwa Julai 2, mwaka huu.
“Najua wapo wanachama wenye nia ya kugombea ubunge, lakini bado
hawajaandika barua rasmi kuomba, inawezekana wametangaza nia zao huko
mitaani na kwenye redio, lakini hawajafanya hivyo kwa kuleta barua rasmi
ofisini, utaratibu wetu kwenye majimbo yenye wabunge, wasubiri hadi
bunge litakapovunjwa,” alisema na kuongeza hawatakiwi kutangaza
hadharani ila kwa kupeleka barua rasmi ofisini.
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia