ALLIANCE WAIBUKA MABINGWA KOMBE LA CHIPUKIZI

TIMU ya Alliance ya jijini Mwanza imefanikiwa kutawazwa mabingwa wapya wa michuano ya kombe la Chipukizi iliyokuwa ikitimua vumbi mkoani Arusha.

Alliance ambayo ilikuwa ikiwakilishwa na timu mbili za U-12 na U-14 zilifanikiwa kuchukua ubingwa michuano hiyo baada ya kuzifunga timu za Nyota na Future Stars zote za jijini Arusha.

Washindi wa pili katika michuano hiyo walikuwa ni Future Stars wakifuatiwa na washindi wa tatu ambao ni Young Life ambapo walitunukiwa zawadi ya vikombe mbalimbali.

Mratibu wa michuano hiyo,Alfred Itaeli alisema kwamba michuano hiyo itakuwa ikifanyika kila mwaka kwa lengo la kuinua vipaji vy soka la vijana nchini na kuwataka wafadhili mbalimbali kujitokeza kusaidia michuano hiyo.

“Tutajitahidi kuhakikisha michuano hii inafanyika kila mwaka ila tunaomba wadhamini wajitokeze kwa kuwa kuna vipaji vingi sana vya soka hapa nchini”alisema Itaeli

About Woinde Shizza

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 Comments:

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia