MAHAKAMA ya rufaa
imetengua hukumu ya awali iliyompatia ushindi aliyewahi kuwa mbunge wa Jimbo la
Arusha, CCM,Chirstopher Felix Mrema, ya kutalikiana na mke
wake wa ndoa, Milcah Kalondu, raia wa ,Kenya,
waliyefunga naye ndoa mwaka 1973 katika kanisa la Anglikan lililopo Nairobi nchini Kenya , na kuzaa naye watoto watatu .
Katika hukumu hiyo mahakama imemtaka Mrema kumrejea mke wake na kumpatia haki zake zote za msingi na
hivyo ,Milcah , ataendelea kumtambua
Mrema kuwa ni mume wake wa ndoa.
Jopo la majaji watatu wa mahakama ya rufaa, Salumu Massati,
Luanda na Harod Nsekela, ambao wamepitia hukumu hiyo iliyotolewa Novemba 20 mwaka 2009 na Jaji
Kakusulo Sambu, wa mahakama kuu kanda ya Arusha ,iliyompatia ushindi Mrema,na
kutengua uamuzi wa awali.
Milcah Kalondu,
amesema, katika rufani yake hakuridhika
na jinsi hukumu hiyo iliyotolewa na Mahakama kuu kanda ya Arusha, kwa sababu
ilisikilizwa upande mmoja na yeye hakupewa nafasi ya kusikilizwa
Mrema,April 30 mwaka 2009 alifungua kesi namba 1 ya mwaka 2009 ,katika
mahakama kuu kanda ya Arusha ambayo aliiomba mahaka kuvunja ndoa yake dhidi ya
mke wake, Milcah Kalondu.
Amesema kuwa mara baada ya mahakama kuu kanda ya Arusha
katika kesi yamsingi kutoa hukumu iliyompatia ushindi,Mme wake, Mrema ,upande wa Mrema ulikuwa ukimtisha na
kumtaka asikate rufaa juu ya kesi hiyo kwa kuwa ataumbuka kwa mara nyingine ikiwemo kupoteza gharama
kubwa kwa uendeshaji wa kesi.
Milcah ,aliitaka jamii kutokuogopa wenye pesa au vyeo
vikubwa wakati wanapodai haki zao kwani haki haipotei hovyo ila inacheleweshwa
hivyo wasikate tama.
Ameongeza kuwa anakamilisha taratibu za kufungua kesi ya
ugoni dhidi ya mwanamke anayedaiwa
kuishi na Mrema kama mke ambaye wameishi naye ,baada ya kutokuelewana mwaka 2007 hatua iliomfanya ,Mrema,ahame
nyumbani na kwenda kuishi na mwanamke huyo .
Katika kesi hiyo mlalamikaji alikuwa akitetewa na Wakili Dk Ronlick
Mchami ,ambae ,ameipongeza mahakama kwa kumtendea haki mteja wake ambae alikuwa
mbioni kupokonywa haki zake za msingi katika ndoa .
Mrema katika kesi hiyo aliwakilishwa na wakili ,Erick Ngimaryo, wa Ajijini Arusha