Serikali katika wilaya ya Hai imezuia kutumiwa kwa majengo ya shule ya
msingi ya Modio ambayo ilikumbwa na tetemeko la ardhi mwanzoni mwa mwezi
uliopita na kufanya shule hiyo kufungwa kwa muda.
Tetemeko hilo limesababisha majengo ya shule hiyo iliyojengwa mwishoni mwa miaka ya 1930 kuwa na nyufa kubwa na kuta kukatika pamoja na baadhi ya sakafu za madarasa kuwa na mashimo.
Mkuu wa wilaya ya Hai Novatus Makunga ameeleza kuwa tayari majengo hayo yamezungushiwa uzio wa kamba na kuwekwa alama za tahadhari ili kuepusha hatari yoyote inayoweza kujitokeza kwa wanafunzi na wananchi wengine.
Alisema kuwa wanafunzi wa shule hiyo ambao watafunga shule leo ijumaa watapewa uhamisho wa muda kwenda katika shule zilizopo karibu na makazi yao.
Alizitaja shule hizo kuwa ni pamoja na Nkokashu,Kishare,Mweeki,Kibohehe, Mbweera na Tolu.
"Tayari tumeshamwagiza mwalimu mkuu kushirikiana na walimu wenzake kuanisha mitaa ambayo wanafunzi wanaishi ili kurahisisha zoezi la uhamisho kwa wanafunzi,"alisema
Makunga amefafanua kwamba lengo la hatua hiyo ni kuhakikisha kwamba mwanafunzi havuki shule moja kwenda nyingine iliyoko mbali zaidi na eneo analoishi labda kwa sababu maalumu.
Alieleza kuwa walimu wote wa shule hiyo nao watahamishiwa kwa muda katika shule hizo za jirani kutegemeana na mahitaji ya shule.
Makunga ametoa wito kwa wadau mbalimbali wa maendeleo kushirikiana na serikali wilayani humo pamoja na kamati ya shule ya msingi ya mudio katika kukusanya nguvu na raslimali ya kujenga miundombinu mipya ya shule hiyo mapema iwezekanavyo.
Majengo yaliyoonyesha kuathirika zaidi ni pamoja na vyumba viwili vya madarasa,ofisi ya walimu pamoja na bwalo la kulia chakula.

Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia