Afisa habari Ngazi ya Taifa wa Kitengo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC) Bi. Usia Nkhoma akitoa maelezo ya awali kuhusiana na mafunzo hayo yanayolenga kuwawezesha vijana kuwa na uelewa na mbinu juu ya ujasiriamali na namna ya kusimamia biashara zao ili kuongeza uzalishaji hivyo kupambana na kuupunguza umasikini katika ngazi zao kabla ya kumkaribisha Mratibu wa Taifa wa Mradi wa ILO wa Ujasiriamali kwa vijana Bw. Louis Mkuku (kushoto).
Ameongeza kuwa pamoja na kupata uelewa juu ya ujasiriamali mafunzo hayo yanakwenda sambamba na lengo namba 1 la Maendeleo ya Milenia ambalo ni Kupunguza Umasikini, kwa kuwa yatawapatia mbinu zitakazowawezesha kuboresha shughuli zao za kujipatia kipato hivyo kuwa na kipato endelevu.
Mratibu wa Taifa wa Mradi wa ILO wa Ujasiriamali kwa vijana Bw. Louis Mkuku akifungua rasmi mafunzo hayo ambapo ametoa hamasa kwa vijana kutumia vizuri elimu watakayoipata wakati huu wa ujana wao kujenga maisha ya baadae na kuahidi kufuatilia kwa umakini matokeo ya mafunzo hayo na kusema atahakikisha kila mwenye ndoto itatimia kwa usimamizi wa ILO na UNIC.
Pichani Juu na Chini Washiriki wa Mafunzo ya Siku moja ya Ujasiriamali wakisiliza nasaha za mgeni rasmi wakati akifungua rasmi mafunzo hayo.
Bi. Mary France kutoka Best Alternative Consulting and Marketing Company (BEACOM) akizungumzia mada ya Ujasiriamali katika usimamizi wa biashara ambayo ndio sehemu nyingi wafanyabiashara wadogo ndipo wanapokwama kutokana na kutokuwa na uelewa wa kutosha.
Pichani Juu na chini ni Bi. Tusnime Kyando kutoka BEACOM akifundisha kwa nadhiria kuhusu swala la uchambuzi wa biashara na gharama za biashara ambayo mjasiriamali anakusudia kuifanya ili aweze kujua ataanzia wapi na aelekee wapi.
Mshauri kutoka BEACOM Bw. Masudi Kandoro akiwaelezea washiriki wa mafunzo hayo ni namna gani wanaweza kupanga matumizi ya fedha waliyonayo ili iweze kukidhi mahitaji ya wanachotaka kufanya.
Bi. Usia Nkhoma akimkaribisha Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya Wanawake Tanzania Bi. Magreth Chacha (katikati) kuzungumza na vijana wajasiriamali. Kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa Access Insurance Agency Tanzania Ltd. Bw. Gadi Kalugendo.
Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya Wanawake Tanzania Bi. Magreth Chacha akielezea jinsi wajasiriamali wadogo wanavyoweza kupata mikopo katika benki yake, aina za mikopo inayotolewa, vigezo vinavyoangaliwa, taratibu zinazofuatwa na taratibu za marejesho ambapo pia amesema japo benki hiyo inatoa kipaumbele kwa wanawake lakini pia wajasiriamali wanaume wanaweza kujiandikisha na kupata mikopo.
Pichani Juu na Chini baadhi ya washiriki wa mafunzo ya Ujasiriamali wakishiriki kutoa maoni na kuuliza maswali wakati mafunzo hayo yakiendelea.
Ukumbi wa Mikutano wa Shirika la Kazi Duniani ukiwa umefurika vijana kutoka vikundi mbalimbali vya jijini Dar es Salaam wakipata elimu ya mafunzo ya Ujasiriamali yaliyoendeshwa na Kitengo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC) kwa kushirikiana na Shirika la Kazi Duniani (ILO).
Kituo cha habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC) kwa kushirikiana na Mpango wa Shirika la Kazi Duniani (ILO) wa Ujasiriamali kwa Vijana wameandaa mafunzo kwa ajili vijana wajasiriamali.
Mafunzo hayo ya siku moja ya ‘Ujasiriamali kwa vijana wasioko mashuleni’ yamefanyika leo katika ukumbi wa ILO jijini Dar es Salaam na kuhudhuria na vijana wajasiriamali mbalimbali.