Hemed Kivuyo.
Pamoja na mkuu wa jeshi la polisi nchini IGP Said
Mwema kuonyesha jitihada za makusudi za kulitakasa jeshi hilo na kurudi katika
kulinda usalama wa Raia na mali zake,badi jitihada hizo zinaonekana kuwa siyo
lolote siyo chochote.
Mbio ndefu za IGP zinavutwa shati na kurudi nyuma na
baadhi ya askari wasiyo waadilifu na hivyo kushindanisha mbio zao dhidi ya mbio
za kamanda Mwema.
IGP Said Mwema alipoingia katika cheo hicho
alijinasibu mambo mengi ikiwa ni pamoja na `kujidai` kuwa jeshi lake litaenda
kisomi,aliwataka wananchi kusahau yote yaliyopita na kushirikiana na jeshi hilo
katika kutokomeza uhalifu wa aina yeyote.
Mimi ni mmoja kati ya waumini wazuri wa kauli zako nzuri,lakini
kadiri siku zinavyokwenda nakatishwa tamaa na baadhi ya askari wako ambao sioni
sababu ya kutokuwaita `wahuni` hao baadhi ya Askari wako .
Pamoja na kali za IGP bado baadhi ya polisi
wanashiriki katika vitendo vua uhalifu,bado wanapiga raia risasi hovyo,bado
wanapokea rushwa kwa kasi,hili ni jeshi la kisomi?
Inanitisha kuamini kama kweli polisi wanaokabidhiwa
silaha za moto kama wana akili timamu achilia mbali elimu.Hiingii akilini kuona
askari akifyatua risasi hovyohovyo tena kwa mwananchi asiyekuwa na silaha ya
moto,huyu Askari kaenda chuo gani? Huyu Askari gani anafika malai na kuanza
kufuatua risasi kama `majununi` bila kwenda kisomi na kubaini mtandao wa
uhalifu na kukamata wahalifu ili kubaini wengine?
Polisi wasomi na wanaofanya kazi kwa ustadi wa hali ya
juu na usomi’siyo tu wameendelea kuuwa raia wasiyokuwa na hatia kwakuwafyatulia
risasi bali wameendelea kudhihirisha
`upofu wao wa akili` kwakuingia katika nyumba ya mtu asiyekuwa mwalifu na
kumpiga Risasi begani.( hao ndiyo polisi wasomi)
Mwandishi wa habari amepigwa Risasi begani na Askari
baada ya kumwingilia ndani kwake,na kwa mujibu wa polisi,wanadai walielekezwa
kwa Mama mmoja ambaye anahisiwa kuwa mwalifu na hata kuhifadhi wahalifu.
Intelejensia ya Polisi imeshindwa kubaini mtandao wa
wahalifu? Mmeweza kubaini maandamano yasiyo halali tu.`polisi dhaifu`.
Matukio ya kutisha naya kuogofya yanayofanywa na
baadhi ya askari katika vituo vya polisi bado zinarudisha nyuma jitihada za
Mwema za kutaka wananchi kuonyesha ushirikiano kwa jeshi hilo ili liweze
kukabiliana na uhalifu wa aina mbalimbali.
Kutokana na baadhi ya askari kukiuka maadili yao na
sasa kunatafsirika kuwa hukumu ipo mikononi mwao na kituo cha polisi siyo tena
mahali salama kama ilivyokuwa ikitamkwa hapo awali.
Miaka mitatu iliyopita Jijini Arusha vija wawili
waliuawa na polisi huku jeshi hilo likijitetea kuwa watu hao ni majambazi
waliyotaka kuvamia kituo kimoja cha mafuta ,na baada ya kuundwa tuma ilibainika
watu hao siyo majambazi kama polisi ilivyojinasibu. (Polisi dhaifu) ``wamebaki
kula rushwa``.
Mpaka sasa haifahamiki polisi hao wapo wapi na
wanafanya nini ,lakini roho za watanzania hao zilipotezwa na polisi hao na
kuliachia doa.
Jijini Dar es salaam siyo mara moja lakini hivi
karibuni dereva tax mmoja alidaiwa kufa akiwa mokononi mwa polisi na kifo hicho
kilitokea baada ya kuhojiwa kwa saa kadhaa na kuteswa.
Siyo hayo tu kuna matukio mengi ambayo yanadhihirisha
kuwa jeshi hilo linapaswa kujitofautisha na majangili ambayo huwavamia rai wema
na kuwapora na hata kuwaua,wakati mwingine jambazi anaweza kukuingilia kwako
akakubia na kukuachia roho yako,iweje polisi waingine na kuua ama kujeruhi? Tuogope
polisi kuliko majambazi?
`polisi dhaifu` wanaongozwa na fikra mgando.
Kama itatokea majambazi yanavamia wananchi na kuwapora
kisha kuwaachia roho zao zikiwa salama ,basi kuna kila dalili kuwa wananchi
watapoteza imani na polisi ambao hawapori mali zao ila wanafisidi roho zao.
Matumaini hayo yanakuja baada kukutana
na kauli inayosema `` mali inatafutwa na kupatikana lakini siyo roho``
Baadhi ya skari kutoa lugha chafu katika vituo vya
polisi,kuwatesa watuhumiwa na kufanya wanalotaka kwa mtuhumiwa na hata wana
ndugu waliofika kujua kinagaubaga juu ya ndugu yao kushikiliwa ,ni jambo
linaloleta ukakasi katika masikio ya kila anayejua maana ya jeshi hilo na
sheria za nchi.``polisi wanaishi na fikra zilizokufa``
Polisi bado wanafanya matukio ya kudhalilisha raia
wema wanaotuhumiwa na hata kuwabambikia tuhuma .``jeshi la polisi limekosa
weledi``.
Hali ya wananchi kuteswa,kutolewa maneno ya lugha
chafu,kubambikiwa kesi na hata kupotezewa maisha wakiwa katika vituo vya polisi
kama ilivyotokea siku za karibuni,inazidi kuifanya jamii ipoteze imani na jeshi
hilo na hata IGP Mwema mwenyewe ambaye anapaswa kuonyesha jitihaza za
kuondokana na hilo kwa vitendo na kwa matukio hayo mpaka sasa IGP MWEMA
unapaswa kuachia ngazi na ukafanye shughuli nyingine. `haiingii akilini kwa
polisi aliytoka chuo kwenda kinyume na maadili kupitiliza alafu jeshi likakaa
kimya..`Abadan`
IGP kuna madhambi mengi yanafanywa na baadhi ya polisi
wako ,wewe huwezi kuwajua ,sisi tunawajua na kuwaona huku mitaani/kuna asakri
mmoja (trafiki) mmempa pikipiki kama unahitaji jina lake ntakupa,sina hakika na
kiwango chake cha elimu lakini nachoweza kusema kwa lugha nyepsi kuwa Askari
huyu ni kielelezo cha `upuuzi` wa baadhi ya Askari ndani ya jeshi hilo.
Pamoja na ujana wake unaomwezesha kufanya kazi kwa bidii
na kufuata maadili,lakini amekuwa kama ameingiwa `maruhani` ya kupokea rushwa
na `uzinzi`
Ndiyo jamii ya walewale waliyomfyatulia Risasi
Mwandishi,sisitaji kutafuta Kiswahili kingine zaidi ya `wahuni` wachcahe ndani
ya jeshi la polisi.
Ninaposema hivyo namaanisha kuwa IGP Mwema ana wajibu
na anapaswa kuwajibika,kwanini Askari wanaingia nyumba ambayo hawakuelezwa? Wamesomea
wapi? Kwanini aingie na kufyatua risasi? Alikuwa anakabailiana na wanamgambo wa
`TALIBANI? Aliingia katika kambi ya M23? Aliingia katika mapango ya Torabora?
Tulitaka kuporwa ziwa nyasa? ``Huu ni upuuzi`` hatupaswi kukaa kimya likapta
hivihivi ni lazima IGP MWEMA awajibike
kwakuwa siyo tukio la kwanza Jeshi lake kwenda kinyume na maadili ya jeshi la
hata katiba ya Nchi.
Mpaka sasa pamoja na jitihada za wakuu
mbalimbaliu wa jeshi hilo bado polisi wanahusika na kupoteza maisha ya raia
wema wanapokuwa chini ya himaya yao ,jambo ambalo linaweza kusababisha
machafuko kama wananci nao wataishiwa uvumilivu.
Imani iliyoanza kurejea kwa wananchi dhidi ya jeshi
hilo inaanza kutoweka siku hadi siku hasa kutokana na vitendo viovu
vya baadhi ya polisi ambao hatuoni hatua zozote wanazochukuliwa.
Askari `mkora` na `muhuni `atafanyakazi hiyo kihuni na
kikora kisha kusababisha maisha ya wananchi kupotea kama ilivyo hivi
sasa.Suala la wananchi ambao wanapelekwa katika vituo vya polisi na
baadaye kutolewa taarifa za kupoteza maisha siyo suala la mzaha kama polisi
wanavyolichukulia kutokana na ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu na sheria . `IGP
NAKUHESHIMU..NAOMBA UONDOKE TAFADHALI..
Nasema hivyo kutokana na hatua zisizoridhisha ambazo
polisi inachukua kwa waajiriwa wake pindi wanapofanya makosa kama hayo na hivyo
kuzidi kuongeza idadi ya matukio kama hayo. KWANINI? IGP NAKUHESHIMU SANA
,NAKUPENDA ,NAPENDA UTENDAJI WAKO ILA HAPA TULIPOFIKA NAOMBA UTAFUTE KAZI NYINGINE TAFADHALI…MUOMBE
RADHI AMIRI JESHI MKUU KISHA UMUOMBE KUACHIA NGAZI..NIPO TAYARI KUKUSAIDIA
KUOMBA HILO KWA RAIS WETU MSIKIVU.
Toka awali jeshi hilo linafanya makosa katika kuajiri
vijana ambao hukaa katika mafunzo ya muda mfupi ambayo ni ya miezo sita kisha
kupelekwa mikoani ,tayari kwakuanza kazi na hapohapo hujifunza kazi
kwakuwakamata vijana katika miji mbalimbali ili kupata uzoefu wa kazi.
Kama kijana alilelewa nyumbani kwao na akawa ni
`mvuta`bangi`asiyekuwa na heshima kwa mkubwa wala mdogo ,akawa ni mwenye kutoa
maneno yenye lugha chafu na sugu wa tabia mbovu ,sidhani kama miezi sita
inaweza kubadilisha tabia yake ya uvutaji bangi na kutoa maneno yenye ukakasi
kwa jamii alafu tukategemea miezi sita itarekebisha tabia yake chafu.
Na ndiyo maana kuna baadhi askari ambayo hukaa katika
vituo vya polisi lakini ni watumiaji wa mihadarati ,ni wasiyo na heshima na
wenye kutoa lugha chafu kwa raia waliyostaarabika.
Haishangazi sana kusikia polisi wameshiriki kupoteza
maisha ya raia mwema aliyefikishwa kituoni kwa kosa la ajabuajabu lisilo na
kichwa wala miguu.
`.
Wananchi hawa hawa wa Tanzania wanateswa na wahalifu
,wanateswa na umasikini,wanateswa na ahadi zisizotekelezeka zinazotolewa na
wanasiasa na bado pia wateswe na polisi ! Sasa watanzania watakosa pakukimbilia
pamoja na amani iliyopo .
Amani bila kuwepo amani ndania ya mikono inayoitwa
salama ya jeshi la polisi siyo amani timilifu.
Watanzania wana moyo hawana jiwe,mengine
wapunguziwe
Abadana, tusiwaache polisi wacheze na maisha ya raia
wema watakavyo.IGP Mwema sasa uachie ngazi kwa kuhifadhi heshima
yako. KWA MUSTAKBALI HUU SIYO SABABU YA ASKARI HAO
WACHCAHE KUENDELEA KULITUMIKIA JESHI LA POLISI,HAO SIYO POLISI BALI NI
MAJAMBAZI”
0752 250157.
0 Comments
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia