Aliyekuwa
mbunge wa jimbo la Arusha mjini Godbless Lema akiwa anawashukuru
wanachini na wadau ambao walifanikisha ununuzi wa vyombo vya chama mkoa
wa arusha wakati walipokuwa wameudhuria kwenye eventya M4C-JOIN THE
CHAIN iliyofanyika katika ukumbi wa hotel ya snowcrest jijini Arusha
Lema akiwa na baadhi ya wanachama
ambao ni wadau wakubwa wa chama cha demokrasia na maendeleo chadema
ambapo alisema kuwa wadau hawa wanatarajia kuingia katika majimbo
mbalimbali hapa nchini kwa ajili ya kuwaletea watanzania ukombozi
Hawa ndo wanakamati waliofanikisha ununuzi wa vyombo vya M4C JOIN THE CHAIN
viongozi wa chama mbalimbali wa mkoa wa Arusha chadema waliuthuria sherehe hii
wadau
mbalimbali waliuthuria katika shughuli hii ya uchangiaji wa vyombo vya
muziki ambapo vilipatikana na uchangiaji wa gari la kubebea vyombo hivyo
ambapo ambapo wageni waliouthuria katika shughuli hii waliaidi kutoa
shilingi milioni 27 kwa ajili ya ununuzi wa gari lakununulia gari na
wewe mdau kama ukiguswa unaruhusiwa kutoa fedha kwa ajili ya ununuzi wa
gari hili ambalo ni kwa ajili ya kuendesha gurudumu M4C JOIN THE CHAIN
unachotakiwa kufanya ni ufike tu katika ofisi za chama cha demokrasia
namaendeleo zilizopo mkoani arusha na utoe mchango wako
katika shughuli hiyo vinywaji vilikuwa vya kumwaga
Mwanadada
Aminata Saguti yeye alitoa mada ila kilio chake kikubwa kilikuwa ni
kwawanawake aliwasihi wanawake watoe dhana ya woga na waanze kazi
wajiamini nawasiogope kugombea nafasi mbalimbali uongozi katika vyama
nahata nchi pia alisemakuwa yeye binafsi anajiamini na anampango wa
kugombea jimbo moja lililopo mkoani Tanga ifikapo mwaka 2015 kwani jimbo
ilo limekuwa likiendeshwa kwa muda mrefu na watu ambao hawajawasaidia
wananchi kitu chochote na wananchi wa jimbo hilo wanazidi kuteseka kila
siku japo kuwa wanambunge wao
mbunge
wa jimbo la Arumeru magharibi Joshua Nasaari akibadilishana mawazo na
aliyekuwa mbunge wa jimbo la Arusha mjini wakati shughuli ikiendelea
ambapo mbunge nassari yeye alitoa shilingi milioni mbili kwa ajili ya
ununuzi wa gari la kubebea vyombo vya muziki
kulikuwa pia na nyimbo zachama cha
demokarasia na maendeleo zinapigwa ivyo kilammoja alionyesha furaha yake
ya kucheza na kufurahia chama chake
pia katika shuhuli hii kulikuwa na watoa mada mbalimbali kuhusianana
mapinduzi mwanadada Kaithari Mohamed ni mpiganaji wa chama cha
demokrasia namaendeleo chadema yeye aliwahamasisha wanawake kujitambua
nakujua haki zao nanini maana ya mapinduzi alisema kuwa mwanamke asifiwi
kwa uzuri wa nje ,gari alilonalo ,nyumba aliyonayo wala umaarufu alio
nao bali ni nini alichoifanyia jamii iliyo mzunguka hivyo aliwasihi
wamama wajitokeze kwa wingi kupigania haki zawatanzania na wajitambua
huku akikumbushia kuwa ata nelson mandella alisaidiwa na mke wake ndo
maana akashinda na uhuru ukapatikana hivyo wanawake wanaweza na sio
mpaka wawezeshwe bali wanaweza wenyewe
katibu wa chama cha demokrasia na maendeleo chadema mkoa wa arusha Amani Golugwa |
Kwaupande wake Katibu wa mkoa Chadema
Amani Golugwa aliwashukuru sana wadau wote ambao wameuthuria na
kushiriki katika shughuli hii ya kuchangia vyombo pamoja na kuchangia
gari lakubebea vyombo na alibainisha kuwa wakati huu ni wa mabadiliko
wanafanya kazi kwakusonga mbele na hawatakubali kurudishwa nyumba huku
akibainishakuwa wakati huu sio wakuulizana nani mwizi bali ni wakati wa
kukamata mwizi nakufanya kazi tu
Alisema kuwa swala la mabadililiko ni
mpango wa mungu hivyo hakuna mtu yeyote ambaye anawezakuzuia mipango wa
mungu aku akisema kuwa wanajua itachukuwa muda lakini lazima mabadiliko
yatatokea tu.
Aliseongeza kuwa kwakipindi hichi
wameamua kuanzisha M4C JOIN THE CHAIN hiii ikiwa ni njia ya kuleta
mabaidiliko huku akisema kuwa wanataka wanyakuwe majimbo yote ya mkoa wa
arusha
"unajua tunataka tunyakuwe majimbo
yote ya mkoa wa arusha nakwanza kabla ya kuyachukuwa tunataka tuanze
kuwaonyesha wananchi katika baadhi ya halmashauri tulizo zichukuwa
ambapo alisema kuwa wao kama chadema mkoa wa Arusha wanamiliki
halmashauri mbili ambayo ni halmashauri ya meru pamoja na karatu ambapo
alisema hizi ndo anataka ziwe za mfano katika kuleta maendeleo.
Alifafanua kuwa vyombo vya mziki
vilivyonunuliwa (pa system)viligharimu kiasi chashilingi milioni 14 na
laki sita ,huku kiasi cha shilingi milini 27 zikiwa ni ahadi kwaajili
ya gari na keshi ikiwa ni shilingi milioni moja
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia