KAMPUNI YA UTALII KIROYERA TOURS YAPATA TUZO JIJINI DAR ES SALAAM KATIKA HOTEL YA BLUE PEARL UBUNGO JANA.


Mr_kalikawe akiwa na binti yake mbunifu wa maavazi Bi Kemi Kalikawe.

Wasalaam

Mkurugenzi wa Kiroyera tours Bi Mary Kalikawe amekuwa ni mmoja wa Wanawake kumi Tanzania ( Women of Determination) katika sector ya Utalii na kuibeba kampuni ya Utalii ya Kiroyera Tours kupata tuzo hiyo usiku wa jana pale Dar es slaam katika hotel ya Blue Pearl Ubungo. Usiku wa jana ulikwa wa furaha kwa wanakiroyera tours.
Sherehe hiyo iliyowakusanya wafanyakazi toka Kiroyera tours head office ya Bukoba, na wafanyakazi wa kiroyera tours Mwanza office iliyopo Delux Mwanza pamoja na wafanyakazi wa kiroyera tours wa office ya Dar es salaam kinondoni studio wali ungana na wadau mbalimbali katika kumpongeza Mkurugenzi wa kampuni hii kwa kutambuliwa na kupata tuzo hii kati ya wanawake kumi bora Tanzania

Sherehe ya tuzo hii imefanyika jana tarehe 1 December iliyondaliwa kwa udhamini mkubwa wa kampuni ya usafirishaji ya vifurushi ya DHL. Kiroyera tours inajivunia kutambulika kitaifa na kimataifa kwani tangu ianzishwe imeshapata tuzo saba mpaka sasa na ndio maana wanajulikana kama PRIVATE AWARD WINNING COMPANY.
Tukikukumbusha tumeshapata tuzo mwaka 2004 - Millenium Tourism Award in Madrid Spain, Mwaka 2005-world bank top 10 Pan African Women Inventor and innovator award in Ghana, 2006 UN Habitat Mashariki Innovations in Local Gogovernance in Nairobi Kenya, 2006 ZEZE award ( Cultural promotion Excellence award in Dar es salaam, 2007 SNV ( Zonal Governance Award) in Mwanza, 2007 - Tanzania chamber of commerce (SME) in Dar es salaam na sasa 2012 Women of determination Award special fr Managing Director of Kiroyera Tours)

Katika sherehe hizi kuna wanawake wengine waliopata tuzo katika sector za Elimu, Ubunifu, Usafirishaji hapa kuna mama anayegonga gia kwenye Bus kubwa ya Shabib kati ya Dodoma na Dar es salaam. Ukweli waandaajii wa Tuzo hizi walifanya kazi ya kuzunguka Tanzania nzima na kuowaona wanawake wanaopashwa kupongezwa kwa kazi zinazoonyesha ubunifu na determination kubwa na kuwapa tuzo. Wanawake wanaweza!!

Kiroyera Tours inawaomba ushirikiano hasa kwa Watanzania kuingia katika sector hii inoyotoa ajira kwa watu wengi kwa kusomea na kuwekeza katika sector hii ya utalii

Meneje wa kampuni hii Bw Willam Rutta akijulikana sana kwa jina la Willy Kiroyera alimbatana na Mzee Super anawaomba wakazi wa kanda ya ziwa kutumia usafiri rahisi wa fast jet kwa kutoka Mwanza - Dar na Dar Kilimanjaro wahi nafasi.
kwani ni nafuu na anasema kiroyera tours imetumia usafiri huu na sasa ukitaka tiketi hizo tafadhali wasiliana nasi tutakupatia tiketi kupitia o fisi yetu ya Dar es alaam kwa kuanzia shi110,000 return mwaza- dar Mwanza au elfu 42,000- 97.000/= iwe sehemu utalii wa ndani kwani wafanyakazi wa kiroyera tours sasa wanatumia fast Jet kwa safari zao.

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

Previous Post Next Post